Venezuela, waachilieni wafungwa na msikilize matakwa yao:Bachelet

22 Juni 2019

Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akizungumza katika mwisho wa ziara yake ya kwanza nchini Venezuela hii leo , ametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuwaachilia watu wote wanaoshikiliwa kwa kuandamana kwa amani . Michelle Bachelet pia ametangaza kwamba timu kutoka ofisini kwake itasalia mjini Caracas mji mkuu wa nchi hiyo ili kufuatilia hali ya haki za binadamu

Kamishina mkuu aliwasili katika taifa hilo la Amerika Kusini Jumatano kwa mwaliko wa serikali ya Rais Nicolas Maduro,bada ya kuelezea hofu yake kuhusu hotuba iliyotolewa kwenye Baraza la Haki za Binadamu mwezi  Machi kuhusu “kuzorota vibaya kwa hali ya haki za binadamu nchini humo kwa ujumla na kuelendea kuwaharamisha watu wanaoondamana kwa amani na kuwakamata.”

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa usiku kwenye uwanja wa ndegewa Maiquetia  Bi. Bachelet ambaye ni Rais wa zamani wa Chile amesema serikali ya Venezuela imekubali timu mpya ya OHCHR “itatoa msaada wa kiufunzi na ushauri na itaendelea kufuatilia hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo.”

© UNHCR/Santiago Escobar-Jarami
Kwa wastan wakimbizi 1650 wa Vinezuela wanaendelea kuwasili kila siku Equador

Akizungumzia ziara hiyo Bi. Bachelet amesema “Katika mikutano yang una waathirika na familia zao , kubwa wanalolihitaji ni haki dhidi ya ukiukwahi mkubwa wa haki za binadamu ambao hawakusita kuuweka bayana na unauma. Ni matuimaini yangu kwamba tathimini yetu , ushauri na msaada vitasaidia kuimarisha hali ya kuzuia utesaji na firsa za kupata haki Venezuela. Serikali pia imekubali kwamba timu yangu itahakikishiwa fursa ya kuingia kwenye vituo vya mahabusuili kuweza kufuatilia hali na kuzungumza na mahabusu wanaoshikiliwa.”

Bachelet amekutana na Rais Maduro na mawaziri wengine wa ngazi za juu pamoja na kiongozi wa upinzani Juan Guaido,ambaye mwezi Januari mwaka huu alijitangaza kuwa Rais wa taifa hilo hatua iliyokuwa chachu ya mgogoro mkubwa wa kisiasa na kuligawa mapande taifa hilo ambalo sasa limeshuhudia watu zaidi ya milioni 4 wakifungasha virago na kuvuka mpaka kukimbia hali tete na kuingia nchi jirani kusaka usalama.

Pia nimekutana na waathirika wa ukiukwaji wa haki za binadamu na familia zao .Mwanaume ambaye alielezea kuhusu kaka yake aliyepitia utweswaji, udhalilishaji na mauaji katika mikono ya askari wa FAES wakati wa msako nyumbani kwake na familia nyinyo zilizoghubikwa na hofu na huzuni ambazo wapendwa wao walipoitia mateso kama hayo na kuishia kifo. Machungu ya mama ambaye mtoto wake wa miaka 14 alipigwa risasi na kuuawa tarehe 30 Aprili makwa huu wakati wa maandamano, na watu waliopitia mateso makubwa mahabusu”

Kamishina Mkuu amesema pia amekutana na “waathirika wa ukatili dhidi ya wafuasi wanaounga mkono serikali. Mama ambaye mtoto wake wa kiume mfuasi wa serikali ambaye alitiwa kiberiti na kuwashwa moto wakati wa maandamano yam waka 2017 na kulazimika kuugua hospitali kwa siku 15 akiwa katika mauamivu makali kabla ya kufariki dunia.”

Picha na UN/Laura Jarriel
Michele Bachelet , Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa , akizungumza na waandishi wa habari 26 Septemba kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York

Amesema wote hawa wametoa ushahidi wa “jinsi gani hali ya haki za binadamu nchini Venezuela iilivyozidi kuwa mbaya ikiweko katika haki ya chakula, maji , huduma za afya, elimu na haki zingine za kiuchumi na kisiasa.”

Takriban asilimia 70 ya bajeti ya serikali hivi sasa inakwenda kwenye program za kijamii kwa ajili ya wote amesema Bi. Bachelet , hata hivyo amesema wamesikia kutoka kwa Wazenezuela ambao wameajiriwa wengi wao katika sekta za umma wakisema wanakabiliwa na wakati mgumu kumudu huduma za madawa na chakula cha kutosha.

Kuporomoka kwa huduma za afya ni mtihani

Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu amesema hali ya afya inaendelea kuwa mtihani mkubwa akigusia kuongezeka kwa gharama kutopatikana kwa madawa na sasa ongezeko la mimba kwa vigori na huku vifo vya kina mama na watoto vikiendelea kuongezeka.

“Nimetoa wito kwa serikali kuhakikisha kwamba takwimu muhimu zinzohusiana na huduma za afya na haki zingine za kiuchumi na kijamii zinawezeshwa katika sekta zote ili kutathimini ipasavyo kwa usahihi na kushughulikia changamoto.”

UNHCR/Stephen Ferry
Wakimbizi na wahamiaji kutoka Venezuela wakiwa wamelala mbele ya kituo cha mabasi mjini Maicao. Colombia. Hali ni mbaya kiasi husababisha wakimbizi kuibiwa mali zao na hata kubakwa.

Akiainisha kuimarishwa kwa hivi karibuni kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko mashinani nchini humo amesema amejadiliana na wahusika haja ya kushughulikia mizizi ya migogoro , wakati huohuo kuweka bayana wasiwasi uliopo wa athari za vikwazo vilivyowekwa na Marekani kwenye mafuta yanayosafirishwa nje kutoka nchini humo, na biashara ya dahabu ambavyo vinachochea hali mbaya ya kiuchumi iliyokuwepo kuwa mbaya zaidi.

Ametoa wito kwa viongozi katika kila nyanja “kutafuta njia za kuwapunguzia wananchi madhila ,mgogoro huu unaweza kutatuliwa tu kupitia njia zenye maana, ushiriki na ushirikishwaji wa wadau wote.”

Hatma ya Wavenezuela zaidi ya milioni 30 ipo mikononi mwa utayari wa uongozi wa serikali na uwezo wake wa kuweka haki za binadamu mbele ya maslahi binafsi, imani na hamasa ya matakwa ya kisiasa au kuelewa na kutambua wasiwasi wa taifa baada ya miaka kadhaa ya uozo na msukosuko mbao unatoa mwanya kwamba muafaka wowote wa kisiasa unawezekana.

“Kusimamia mitazamo na misimamo yao kila upande , kutazidisha mzozo na watu wa Venezuela hawawezi kumudu kudorora zaidi kwa hali nchini humo.”Amesema Bi. Bachelet

Na hatimaye”Natoa wito wa hatua madhubuti kuelekea muafaka, kuweka malengo kwa ajili ya ushinfi wa muda mfupi na faida za muda mrefu kwa taifa zima, Akigusia majadiliano baina ya serikali na upinzani yanayoendelea nchini Norway amesema :mazungumzo yanaweza kufanikiwa endapo tu yatakuwa jumuishi, na wahusika watachukua hatua kutokana na uharaka wake ili kuhakikisha yanafanikiwa.

 

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter