Skip to main content

Mlinda amani kutoka Burkina Faso ashinda Tuzo ya Afisa wa Polisi Mwanamke wa Umoja wa Mataifa mwaka 2022

Afisa Mkuu Alizeta Kabore Kinda wa Burkina Faso, ambaye kwa sasa anahudumu katika Misheni ya Umoja wa Mataifa ya Kuimarisha Uimarishaji wa Mipaka Mbalimbali nchini Mali (MINUSMA) atapokea Tuzo ya Afisa wa Polisi Mwanamke wa Umoja wa Mataifa 202
UNPOL
Afisa Mkuu Alizeta Kabore Kinda wa Burkina Faso, ambaye kwa sasa anahudumu katika Misheni ya Umoja wa Mataifa ya Kuimarisha Uimarishaji wa Mipaka Mbalimbali nchini Mali (MINUSMA) atapokea Tuzo ya Afisa wa Polisi Mwanamke wa Umoja wa Mataifa 202

Mlinda amani kutoka Burkina Faso ashinda Tuzo ya Afisa wa Polisi Mwanamke wa Umoja wa Mataifa mwaka 2022

Masuala ya UM

Umoja wa Mataifa umemtangaza Afisa Mkuu Alizeta Kabore Kinda kutoka nchini Burkina Faso kuwa mshindi wa Tuzo ya Afisa wa Polisi Mwanamke wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2022.

Taarifa hiyo iliyotolewa hii leo jijini New York Marekani imesema tuzo hiyo itatolewa wakati wa Mkutano wa tatu wa Wakuu wa Polisi wa Umoja wa Mataifa UNCOPS, utakaofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kuanzia tarehe 31 Agosti hadi 1 Septemba 2022.

Mkutano huo wa UNCOPS utawaleta pamoja mawaziri, wakuu wa polisi, na wawakilishi wakuu wa mashirika ya polisi ya kikanda na kitaaluma ili kushiriki katika kuimarisha amani ya kimataifa, usalama na maendeleo kupitia kuunganisha nguvu pamoja katika kutekeleza majukumuya polisi wa kitaifa na Umoja wa Mataifa.

Bettina Patricia Boughani wa Ufaransa (katikati) ni Meja Jenerali katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA). Ameongoza kitengo cha polisi cha ujumbe huo (UNPOL) tangu 2021. Akitoa salamu kwa wanajeshi.
@MINUSMA-POL
Bettina Patricia Boughani wa Ufaransa (katikati) ni Meja Jenerali katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA). Ameongoza kitengo cha polisi cha ujumbe huo (UNPOL) tangu 2021. Akitoa salamu kwa wanajeshi.

Kuhusu mshindi huyo wa Tuzo wa mwaka 2022

Afisa Mkuu Kinda anahudumu kama msimamizi wa kitengo cha kijinsia katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuimarisha Utulivu nchini Mali MINUSMA, ambapo anasaidiana na Vikosi vya Usalama vya nchini Mali katika eneo la Menaka ili kukuza na kuboresha uelewa wa jinsia, ulinzi wa watoto, haki za binadamu na kiraia pamoja na masuala ya ulinzi. 

Kufuatia juhudi zake, waathirika wengi zaidi wa unyanyasaji wa kingono na kijinsia wanajitokeza kuripoti kesi zao kwa mamlaka za mitaa na kupokea huduma ya matibabu maratatu au zaidi kwa mwezi ikilinganishwa na kipindi ambacho hakuwepo katika nafasi hiyo.

Juhudi zake pia zimelenga katika kupanua wigo wa kuongeza idadi ya wasichana shuleni na kupunguza ndoa za utotoni.

Alipopokea habari za tuzo yake, Kinda alielezea kuwa "Natumaini kwamba itawatia moyo wanawake na wasichana kote ulimwenguni kufuata kazi ya polisi licha ya dhana potofu za kijinsia ambazo mara nyingi huhusishwa na taaluma: kwamba wanaume wanafaa zaidi kutekeleza sheria na kulinda jamii yetu."

Naibu Katibu Mkuu wa Operesheni za Amani Jean-Pierre Lacroix amemsifu mshindi huyo kwa kusema “Kazi za Afisa Mkuu Kinda ni mfano mzuri wa jinsi ushiriki wa polisi wanawake katika operesheni za amani unavyoathiri moja kwa moja uendelevu wa amani kwa kusaidia kuleta mitazamo tofauti wakati wa kufanya kazi yetu kuwa shirikishi zaidi." 

Lacroix ameongeza kuwa “Kupitia matendo yake, anajumuisha uwakilishi zaidi, huduma ya polisi yenye ufanisi ambayo ina vifaa vya kuhudumia na kulinda umma.”

Utendaji kazi wake ni mzuri toka enzi na enzi

Kazi ya Afisa Mkuu Kinda imejikita katika kulinda na kukuza haki za wanawake na watoto, ikiwa ni pamoja na kati ya 2013 hadi 2015, alipokuwa kitengo cha jinsia katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO

Mshauri wa Polisi wa Umoja wa Mataifa Luis Carrilho amesema afisa Mkuu Kinda ameonesha ubunifu na kujitolea katika kushughulikia mahitaji maalum ya usalama ya jamii anazohudumia "Yeye na timu yake wanasaidia kuongeza uaminifu kati ya mamlaka za mitaa za Mali na jamii, ambayo inafanya kazi ya Polisi ya Umoja wa Mataifa kuwa na ufanisi zaidi na watu salama."

Katika nchi yake ya alipozaliwa Burkina Faso, alifanya kazi hizi ndani ya Wizara ya Usalama na Brigedi ya Kikanda ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto, kitengo cha polisi wa kitaifa, kama mpelelezi wa unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji.

Mlinda amani wa MINUSMA akiwa kwenye doria huko Gao nchini Mali
/Marco MINUSMADormino
Mlinda amani wa MINUSMA akiwa kwenye doria huko Gao nchini Mali

Kuhusu Tuzo ya Afisa Polisi Mwanamke wa Umoja wa Mataifa

Tuzo ya Afisa wa Polisi Mwanamke wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa ilianzishwa mwaka 2011 ili kutambua mchango wa kipekee wa maafisa wa polisi wanawake katika operesheni za amani za Umoja wa Mataifa na kukuza uwezeshaji wa wanawake.

Takriban Polisi 10,000 wa Umoja wa Mataifa wameidhinishwa kuhudumu katika operesheni 16 za amani za Umoja wa Mataifa, ambapo wanafanya kazi ya kuimarisha amani na usalama wa kimataifa kwa kuunga mkono nchi mwenyeji katika mizozo, maisha baada ya mizozo na hali nyingine za mgogoro.

Wanawake wanajumuisha zaidi ya asilimia 19 ya maafisa wa polisi wa Umoja wa Mataifa wanaohudumu kwa sasa. Ushiriki wa wanawake katika Polisi wa Umoja wa Mataifa umeongezeka maradufu tangu 2015.

Kufikia leo, UNPOL tayari imefikia malengo ya 2025 yaliyowekwa katika Mkakati wa Idara wa Usawa wa Kijinsia kwa makundi yote ya wafanyakazi. Maafisa wa polisi wanawake ni asilimia 31.5 ya maafisa wa polisi waliotumwa kibinafsi na 14.6% ya wanachama wa Vitengo Vilivyoundwa vya Polisi. 

Wanawake pia wanaongoza nusu ya vitengo vya Polisi vya Umoja wa Mataifa katika uwanja huo, ikiwa ni pamoja na operesheni za amani za Umoja wa Mataifa huko Abyei, Cyprus, Kosovo, Mali, Sudan Kusini na Sudan.