Chuja:

tuzo

UNEP

Mshindi wa tuzo ya mazingira wa UNEP 2021 kutoka Uganda azungumzia kazi anazofanya

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira duniani, UNEP wiki hii Jumanne ya tarehe 07 limewatangaza washindi wanne wa tuzo yake ya juu kabisa ya mazingira ijulikanayo kama “champions of the Earth Award” kwa mwaka 2021. Mabingwa hao walichaguliwa kutokana na mchango katika mazingira na uongozi wao katika kuendeleza hatua za ujasiri na madhubuti kwa niaba ya watu wengine wa sayari dunia. Dk Gladys Kalema-Zikusoka wa Uganda ni mmoja wa tuzo hiyo ya UNEP katika kipengele cha Sayansi na Ubunifu.

Sauti
3'39"

09 Novemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo miongoni mwa taarifa utakazo sikia leo ni pamoja na:- 
Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Nepal Sangya Malla anayehudumu katika ujumbe wa Umoja huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo -DRC, MONUSCO ameshinda tuzo ya Afisa Polisi Mwanamke wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2021

Sauti
14'57"
Picha kutoka kwenye video wakati Maria Ressa alipokuwa akishiriki mkutano wa UNESCO kuhusu uhuru wa vyombio vya habari. (Mei 4, 2020)
UNESCO

UNESCO leo imekabidhi tuzo ya Guillermo Cano kwa Maria Ressa

Mwandishi wa habari wa uchunguzi wa Ufilipino leo ametunukiwa tuzo  ya heshima kwenye hafla iliyoandaliwa iliyoandaliwa na Serikali ya Namibia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO katika mji mkuu Windhoek, nchini Namibia ambako wataalamu wa vyombo vya habari wanataka hatua za dharura zichukuliwe dhidi ya vitisho na kudhoofishwa kwa uhuru wa habari kote ulimwenguni.