Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Moto kanisani Misri, Guterres atuma rambirambi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
UN Photo/Violaine Martin (file)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.

Moto kanisani Misri, Guterres atuma rambirambi

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea masikitiko yake kufuatia vifo na majeruhi vilivyosababishwa na moto kwenye kanisa la madhehebu ya wakristo wa kikoptiki huko nchini Misri hii leo jumapili.

Taarifa ya  Msemaji wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo jijini New York, Marekani imemnukuu Katibu Mkuu akituma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha na serikali ya Misri huku akitakia ahueni ya haraka majeruhi.

Moto huo uliitokea wakati wa ibada kwenye kanisa hilo la Abu Sifin mjini Giza nchini Misri ambapo kwa mujibu wa vyombo vya habari zaidi ya waumini 40 wamekufa na makundi kadhaa wamejruhiwa, wakiwemo watoto.

Inaelezwa kuwa moto uliosababishwa na umeme alianza wakati waumini takribani 5,000 wakiwa kwenye ibada kwenye kanisa hilo lenye ghorofa, na tafrani ilizidi pale ambapo moto huo uliwaka zaidi kwenye eneo la mlango na kuzuia watu kuweza kutoka kwa urahisi.

Idara ya zimamoto iliweze kuzima moto huo lakini hadi sasa chanzo chake halisi hakijaweza kudhihirika.