Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yalaani shambulizi kanisani Burkina Faso

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Burkina Faso wakiwa Ber katikati mwa Mali mwezi Mei 2018.
MINUSMA
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Burkina Faso wakiwa Ber katikati mwa Mali mwezi Mei 2018.

UN yalaani shambulizi kanisani Burkina Faso

Amani na Usalama

Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulio lililofanyika leo kwenye kanisa Katoliki Kaskazini mwa Burkina Faso ambalo limekatili maisha ya watu sita.

Duru za habari zinasema shambulio hilo lililofanywa na mtu mwenye sialaha limetokea kwenye mji wa Dablo,ambao umeshuhudia ongezeko la machafuko  katika miezi ya karibuni.

Wakati wa shambulio hilo kanisa liliteketezwa kwa moto pamoja na majengo mengine kikiwemo kituo cha afya.Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa twitter Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Maria Espinosa, ametoa wito wa wauaji kuwajibishwa. “Hatuwezi kuvumilia chuki. Haki ya msingi ya uhuru wa dini ni lazima iheshimiwe kila mahali.”

Naye Metsi Makhetha, mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Burkina Faso, ametoa ujumbe kupitia twitter yake pia akilaani vikali mashambulizi ya leo Dablo, na kuyaatita ni ya kikatili huku akitoa salamu za rambirambi kwa familia za waathirika na waliopoteza maisha.

Shambulio hilo la risasi limekuja siku chache baada ya tahadhari kutolewa na maafisa wa kibinadamu wa Umoja wa Mastaifa akiwemo Bi. Makhetha kuhusu hali isiyo ya kawaida ya kuongezeka kwa mashambulizi ya silaha Sahel ambayo yanaweka mustakabali wa kizazi chote katika hatari kubwa. “

Machafuko yanasambaa Mali na Niger, lakini pia Burkina Faso na kuna hatari kubwa ya kusambaa katika mataifa mengine ya Afrika Magharibi. Machafuko haya ya karibuni yamesababisha ongezeko la ⅕ ya watu wanaotawanywa nchini humo na katika miezi 12 iliyopita kumeshuhudiwa zaidi ya watu 330,000 walioamua kufungasha virago na kukimbia mbali ya wakimbizi 100,000.

Kwa mujibu wa Bi. Makhetha kundi lkenye silaha lililohamasishwa na ISIS linatishia kuvuruga amani na utamaduni wa muda mrefu wa suluhu ya migogoro ya kijamii.

”Umoja wa Mataifa, mashirika wadau wa kibinadamu na serikali za ukanda huo wameongeza juhudi  za operesheni zao lakini ni lazima tuongeze bidii.”