Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Takriban watu 1000 wamekufa wakati wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania 2021. (Maktaba)

Uchunguzi ufanyike kwa vifo vya waafrika mpakani mwa Morocco na Hispania

SOS Méditerranée/Anthony Jean
Takriban watu 1000 wamekufa wakati wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania 2021. (Maktaba)

Uchunguzi ufanyike kwa vifo vya waafrika mpakani mwa Morocco na Hispania

Haki za binadamu

Umoja wa Mataifa umesikikitishwa na vifo vya waafrika 23 na wengine zaidi ya 76 kujeruhiwa wakati wakijaribu kuvuka mpaka katika ya Morocco na Hispania ili kwenda barani Ulaya kupitia mpaka wa Mellila na Ceuta.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Ravina Shamdasani akiwa mjini Geneva Uswisi imesema tukio hilo lililotokea tarehe 24 juni 2022 linapaswa kuchunguzwa kwa ufanisi na uhuru na nchi zote mbili na wote waliohusi kusababisha vifo na majeruhi wachukuliwe hatua za kisheria na wawajibishwe kama inavyofaa. Mazingira ya vifo Shamdasani amewaambia waandishi wa habari kuwa hii ni idadi kubwa zaidi ya vifo vya wahamiaji kurekodiwa katika tukio moja baada ya miaka mingi na kwamba “Ofisi ya haki za kinadamu imepokwa ripoti za wahamiaji hao kuchapwa na fimbo, kupigwa mateke, kushambuliwa na mawe pamoja na kurushwa na maafisa wa Morocco wakati wakijaribu kuinua waya wenye urefu wa takriban mita Sita mpaka kumi ambao unatenganisha Morocco na Melilla.” Amesema katika harakati hizo za kuwazuia waafrika hao kuvuka askari wa mpakani wa Morocco mia moja na arobaini nao wameripotiwa kupata majeraha. “Tunatoa wito kwa Morocco na Hispania kuhakikisha wanaheshimu haki za binadamu za wahamiaji katika mpaka wao wa pamoja na maafisa walio mpakani waepuke matumizi yoyote ya nguvu kupita kiasi dhidi ya wahamiaji.” Amesema Shamdasani Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia imetaka hatua zote za haraka kuchukuliwa kupitia Jumuiya ya Ulaya, Umoja wa Afrika pamoja na wahusika wengine wa kimataifa na kikanda katika kuhakikisha mipakani kuna utawala bora unaozingatia haki za binadamu. “Hatua hizo ni pamoja na kuhakikisha kuna njia salama za wahamiaji kupita, kufanyika kwa tathmini binafsi za kila mtu anayetaka kupita mpakani, pamoja na kuwahakikishia ulinzi dhidi ya kufukuzwa kwa pamoja au kukamatwa na kuwekwa vizuizini kuholela”. Wahamiaji wengine wakutwa wamekufa nchini Marekani Katika hatua nyingine Ofisi ya Kamishna Mkuu imesema imesikitishwa na ripoti ya kwamba takriban miili ya watu 46 imepatikana huko ndani ya lori huko San Antonio , Texas nchini Marekani ikihisiwa baada ya kuvuka mpaka. Hili si tukio la kwanza la aina hiyo kutokea na kwamba tukio hili linaonesha kuna umuhimu wa kuwa na uchunguzi wa mara kwa mara wa njia salama kwa wahamiaji pamoja na kuhakikisha kuna uwajibikaji wa pamoja kwa wote wanaohusika na usafirishaji wa aina hiyo na kusababisha vifo vya aina hiyo.