Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mwanamke mzee akiwa katika kambi ya wakimbizi wandani nchini Somalia

WHO yatoa vipaumbele 5 kukabiliana na unyanyasaji wa wazee

© UNICEF/Sebastian Rich
Mwanamke mzee akiwa katika kambi ya wakimbizi wandani nchini Somalia

WHO yatoa vipaumbele 5 kukabiliana na unyanyasaji wa wazee

Afya

Leo ni siku ya kuhamasisha kupinga unyanyasaji dhidi ya wazee na katika kuadhimisha siku hii Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO na wadau wake wamechapisha vipaumbele vitano vitakavyosaidia kuzuia na kukabiliana na unyanyasaji wa wazee na hivyo kuchangia katika kuboresha afya, utawi na utu wao.

Taarifa iliyotolewa leo na Etienne Krug, Mkurugenzi wa Idara ya Maamuzi ya Kijamii ya Afya, wa WHO kutoka Geneva Uswisi imesema kutolewa kwa vipaumbele hivyo ni miongoni mwa utekelezaji wa ahadi zilizowekwa kwenye Muongo wa Umoja wa Mataifa wa kuzeeka kwa afya (2021–2030) pamoja na kutekeleza Malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Kila mwaka mtu 1 kati ya 6 walio na umri wa miaka 60 na zaidi hupata aina fulani ya unyanyasaji, huku wafanyakazi 2 kati ya 3 katika taasisi kama vile nyumba za kulea wazee na vituo vingine vya utunzaji wa muda mrefu wakikiri kutenda unyanyasaji katika mwaka uliopita. "Unyanyasaji wa wazee ni ukosefu wa haki, ambao unaweza kuwa na madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na vifo vya mapema, majeraha ya kimwili, sonona, kupungua kwa utambuzi na umaskini" asema Etienne Krug, Mkurugenzi wa Idara ya Maamuzi ya Kijamii ya Afya, WHO.” [scald=250942:sdl_editor_representation] Vipaumbele 1. Kuongeza mapambano dhidi ya ubaguzi wa uzee kwani ndio sababu kuu inayofanya unyanyasaji wa wazee hauzingatiwi sana. 2. Kutengeneza takwimu bora zaidi zitakazoongeza ufahamu wa tatizo 3. Kubuni na kuongeza ufumbuzi wa gharama nafuu kukomesha unyanyasaji wa wazee. 4. Kufanya uwekezaji ukizingatia jinsi kushughulikia shida ni pesa iliyotumiwa vizuri. 5. Kutafuta fedha zaidi kwakuwa rasilimali zaidi zinahitajika ili kukabiliana na tatizo. Kama ilivyokuwa kwa unyanyasaji wa aina mbalimbali, unyanyasaji wa wazee umeongezeka wakati wa janga la COVID-19. Kwa kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu katika nchi nyingi, mwelekeo huu unaokua unatarajiwa kuendelea. Krug amesema “Pamoja na kuenea maeneo mengi duniani lakini unyanyasaji wa wazee haupo katika ajenda ya afya ya kimataifa. Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuzeeka Kiafya 2021–2030 unatoa fursa ya kipekee ya linategemea kutakuwa na ushirikiano wa kiserikali, mashirika ya kiraia, mashirika ya kimataifa, wataalamu, wasomi, vyombo vya habari na sekta binafsi katika kuboresha maisha ya wazee, familia zao na jamii wanamoishi.