Kampeni ya utoaji chanjo ya homa ya mafua makali yaendelea ukanda wa ulaya: WHO
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kanda ya ulaya tangu kuanza kwa msimu wa baridi kali katikati ya mwezi Novemba mwaka 2022 wamebaini kuongezeka kwa wagonjwa wanaolazwa kutokana na magonjwa ya homa ya mafua makali au flu, matatizo ya kupumua na COVID-19. Walio hatarini zaidi kupata maambukizi ya magonjwa hayo ni wahudumu wa afya pamoja na wazee, ndio maana wanaendesha kampeni ya kutoa chanjo.