Janga la COVID-19 limeongeza ukatili dhidi ya wazee: mtaalam wa UN aonya

15 Juni 2021

Wakati mitazamo ya zamani kuhusu uzee tayari inadhoofisha uhuru wa wazee katika kufanya uchaguzi na maamuzi yao wenyewe, janga la COVID-19 limeleta zahma zaidi, dhuluma na kutelekezwa dhidi watu hao, ameonya leo mtaalam huru wa  haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, katika ujumbe wake kuhusu Ulimwengu siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhudu ukatili dhidi ya wazee.

Mtalaam huyo huru Claudia Mahler wa kuhusu kufurahia haki za binadamu za wazee amesema "Ripoti za kusikitisha kutoka kwenye nyumba za kulea wazee katika sehemu tofauti duniani zimeonyesha kwamba wazee wanapuuzwa, kutengwa na kukabiliwa na ukosefu wa huduma za kutosha, zikiwemo huduma za afya, huduma za kijamii na za kisheria".

Kifungo cha COVID-19

Hatua za kuzuia kusambaa na kudhibiti virusi vya corona zimesababisha kuongezeka kwa unyanyasaji wa kijinsia, ukatili na kutelekezwa kwa wazee waliojikuta kifungoni wakiwa wanaishi na wanafamilia na walezi wao.
Licha ya taharuki kubwa juu ya hali hii, changamoto ya kutafuta suluhisho bora, imepokea haijatiliwa maanani, kulingana na mtaalam huyo wa haki za binadamu."Baadhi ya vitendo vya unyanyasaji viliripotiwa huku vituo vya kulelea wazee vikipewa kinga  dhidi ya vifo vitokanavyo na COVID-19 na kuweka vifungu vya mkataba ambavyo vinafuta haki ya kufungua kesi mahakamani, na kufanya usuluhishi kuwa chaguo pekee kwa madai ya ukatili au unyanyasaji", Amesema Bi Mahler.

Wanawake wazee katika moja ya kambi ya wazee inayohudumiwa na serikali nchini Msumbiji.
World Bank/ Eric Miller
Wanawake wazee katika moja ya kambi ya wazee inayohudumiwa na serikali nchini Msumbiji.

Kusaka haki

Mahali pengine, wazee na familia zao walionyesha kukata tamaa na kuchanganyikiwa kutokana na kukosekana kwa uwazi na kujibu malalamiko yaliyotolewa na watoa huduma ya wazee.
Mtaalam huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa “hii inadhoofisha ufikiaji wao wa haki na suluhisho bora", akisisitiza kwamba utu na haki za wazee "hazina tarehe ya kumalizika katikia maisha yao baadaye".
Ufikiaji wa haki unajumuisha haki ya kuwa na kesi , upatikanaji sawa na usawa mbele ya mahakama, na suluhisho la haki na kwa wakati unaofaa kwa ukiukaji wa haki za binadamu.
Ukosefu wa habari za kina na uchambuzi wa kina "hupunguza uwezekano wa kufichua mifumo ya unyanyasaji, ambayo taarifa zake haziripotiwi, na kubaini mapungufu katika hatua zilizopo na pia kutambua hatua madhubuti zinazohitajika ili kutoa ulinzi wa kutosha kwa wazee" , ameongeza mtaalam huyo huru.
 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter