Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wagonjwa wa COVID-19 yaongezeka Kusini mwa Afrika: WHO 

Watu wanapanga foleni kwa ajili ya vitakasa mikono Johannesburg nchini Afrika Kusini.
© IMF/James Oatway
Watu wanapanga foleni kwa ajili ya vitakasa mikono Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Idadi ya wagonjwa wa COVID-19 yaongezeka Kusini mwa Afrika: WHO 

Afya

Wagonjwa wa COVID-19 wanaongezeka kwa wiki ya tatu mfululizo Kusini mwa Afrika wakati huu msimu wa baridi unapokaribia kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.  

Shirika hilo linasema wagonjwa 46, 271 wamerekodiwa katika wiki iliyoishia tarehe 8 Mei 2022, ikiashiria ongezeko la asilimia 32% zaidi ya wiki iliyotangulia.  

Ongezeko hilo limechangiwa zaidi na idadi kubwa ya wagonjwa nchini Afrika Kusini ambapo visa vinavyorekodiwa kila wiki vimeongezeka mara nne katika wiki tatu zilizopita ingawa idadi ya vifo haijaongezeka sana.   

Hali nchini Afrika Kusini 

Kwa mujibu wa WHO Afrika Kusini imeorodhesha vifo 376 katika wiki tatu zilizopita ikiwa ni mara mbili ya iddadi iliyokuwa wiki tatu zilizotangulia. 

Hata hivyo shirika hilo limesema ingawa idadi ya wagonjwa imeongezeka , watu wanaolazwa idadi yao bado iko chini Afrika Kusini takribani asilimia 20 ya idadi iliyokuwa mwezi Desemba mwaka jana mwezi uliokuwa na idadi kubwa zaidi ya wagonjwa. 

Katika majimbo mengine ya Gauteng na KwaZulu-Natal ambako wimbni la sasa la maambukizi ndiko lilibainika kwanza kote idadi ya watu wanaolazwa na vifo vya wagonjwa hospitalini vimeongezeka kwa asilimia kati ya 90 na 100 katika wiki mbili ilizopita ikilinganishwa na siku nne kabla yah apo. 

Kichocheo cha ongezeko la wagonjwa 

Shirika hilo la afya la Umoja wa Mataifa limesema lawama inaelekezwa kwa mlipuko wa virusi vipya ya Omcron ambavyo vilizuka wakati mbinu na masharti ya kujikinga na corona yalikuwa yamelegezwa. 

Tangu mwanzoni mwa mwezi Aprili Afrika Kusini imeorodhesha  wagonjwa 1,369 wa Omicron. 

Mbali ya Afrika Kusini, Eswatini na Nambia pia wameorodhesha ongezdeko la wagonjwa huku nchi zote mbili zikiripoti asilimia 50 zaidi ya wagonjwa wapya katika kipindi cha wiki mbili  zilizopita ukilinganisha na wiki mbili kabla ya hapo imesema WHO. 

Mwenendo wa maambukizi Kusini mwa Afrika 

Milipuko minne ya majanga iliyopita barani Afrika ilitokea katikati na mwishoni mwa mwaka na ikisukumwa zaidi na aina mpya za viruzi vya COVID-19, misimu ya baridi na harakati nyingi za idadi kubwa ya watu kusafiri wakati wa likizo na sikukuu.  

Mwaka 2021, mlipuko wa virusi aina ya Delta ulichangia wimbi kubwa la maambukizi katikati ya mwaka  kuanzia mwezi Mei hadi mwishoni mwa Novemba apapo kukazuka mlipuko mwingine wa Omicron. 

  "Hali hii ya kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa ni ishara ya onyo la mapema ambalo tunafuatilia kwa karibu. Sasa ni wakati wa nchi kuzidi kujitayarisha na kuhakikisha kuwa zinaweza kuchukua hatua madhubuti iwapo kutakuwa na wimbi jipya la janga hili,” amesema Dkt. Abdou Salam Gueye, mkurugenzi wa maandalizi ya dharura na hatua katika ofisi ya WHO Kanda ya Afrika. 

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita nchi za Kiafrika zimeboresha sana hatua zake za kupambana na COVID-19, huku mambo muhimu kama vile ufuatiliaji, upimaji na matibabu yakiimarishwa.  

“Ni muhimu kwamba hatua hizi zidumishwe na kuongezwa haraka iwapo kesi za COVID-19 zitaongezeka zaidi na katika nchi nyingi,”limesema shirika hilo la afya duniani. 

Hatua zinazochukuliwa Afrika 

 WHO inasema bara hilo pia limeongeza mpangilio wa ufuatiliaji wa jeni. Kati ya Januari na Aprili 2021, maabara za Kiafrika ziliripoti kuhusu mlolongo 9,000. Hili ni ongezeko la mara nne hadi karibu 40 000 katika kipindi kama hicho mwaka huu. 

"Kwa uzoefu uliopatikana katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, lazima tufanye njia kuchukua hatua ili kupunguza athari mbaya za wimbi jipya la janga la COVID-19 kwa kuongeza chanjo na hatua za kugundua na kuzuia kuenea kwa virusi lakini pia kutibu wagonjwa. Ili kushinda janga hili, lazima tukae macho. Ukweli mbaya ni kwamba kuridhika dhidi ya ugonjwa huu kutatugharimu sana." amesema Dkt Gueye wa WHO.