Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF imetanabaisha kuhusu hatari kubwa za afya ya akili kwa watoto wa Ukraine

Msichana  kutoka Ukraine akimliwaza ndugu yake wa miaka sita wakati wakijiandaa kuondoka katika kituo cha Romania.
© UNICEF/Alex Nicodim
Msichana kutoka Ukraine akimliwaza ndugu yake wa miaka sita wakati wakijiandaa kuondoka katika kituo cha Romania.

UNICEF imetanabaisha kuhusu hatari kubwa za afya ya akili kwa watoto wa Ukraine

Afya

Wiki kumi baada ya vita kuzuka nchini Ukraine, wasaidizi wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo wamesema kwamba wanaongeza haraka juhudi za kuwapa watoto walio katika mazingira magumu msaada wa kitaalamu na kisaikolojia, huku kukiwa na mahitaji mkubwa ya afya ya akili na hatari zinazoendelea zinazohusiana na uvamizi wa Urusi na ukatili wa kingono na kijinsia.

"Tunatarajia idadi kubwa ya makumi kwa maelfu ya watoto kuathirika na aina zote za ukatili dhidi ya watoto," amesema Aaron Greenberg, mshauri wa ulinzi wa watoto wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika kanda ya Ulaya na Asia ya Kati. 

Hali ni mbaya kwa maelfu ya watoto 

Shirika hilo limesema kabla ya Februari 24, vituo vya watoto yatima vya Ukraine, shule za bweni na taasisi nyingine za vijana, zilihifadhi zaidi ya watoto 91,000, karibu nusu yao ni wenye ulemavu. 

Leo, karibu theluthi moja tu ya idadi hiyo ndio wamerejea nyumbani, ikiwa ni pamoja na wale waliohamishwa kutoka mashariki na Kusini mwa nchi , kulingana na UNICEF. 

"Athari za vita kwa watoto hawa zimekuwa mbaya sana," amesema Bwana. Greenberg afisa wa UNICEF , akizungumza na waandishi wa habari huko Geneva kwa njia ya zoom kutoka Lviv.  

Ameongeza kuwa "Maelfu ya watoto wanaoishi katika taasisi au vituo vya malezi wamerudishwa kwa familia, wengi wao kwa haraka, vita vilipoanza. Lakini wengi hawajapata matunzo na ulinzi wanaohitaji, hasa watoto wenye ulemavu.” 

Kujikwamua na hali hii 

Likilaani ukweli kwamba mamia ya vijana wameuawa katika mashambulizi ya makombora tayari, shirika hilo la Umoja wa Mataifa limeonya kwamba wengine walikuwa wamepatwa na kiwewe kikubwa cha afya ya akili kinachohusishwa na athari za moja kwa moja za vita na vurugu, kimwili na kingono. 

Huku akisisitiza kwamba watoto wengi wataweza kurejea kwenye maisha ya kawaida ikiwa wanaweza kurejea shuleni na kuanza kuona aina fulani ya ukawaida katika maisha yao, Bwana. Greenberg ameongeza kuwa ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kuhakikisha kwamba wafanyakazi wa huduma za kijamii wa Ukraine wamehakikishiwa usalama na kuhimizwa kukaa na kusaidia. 

Amebainisha pia kwamba idadi ndogo, lakini muhimu ya Watoto wataweza  kupata ugonjwa wa msongo wa mawazo kati ya miezi miwili na minne baada ya kupata kiwewe cha vita hivyo. 

"Tangu Februari 24 UNICEF na washirika wetu wamefikia zaidi ya watoto 140,000 na walezi wao kwa huduma za afya ya akili na kisaikolojia," ameendelea kusema na kuongeza kuwa "Lakini idadi kubwa ya hiyo, asilimia 95, ni wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na watoto na wanasaikolojia walio na mafunzo maalum." 

Katika kituo cha hifadhi magharibi mwa Ukraine, watoa mafunzo wakilinda watoto kutoka kwa maeneo ya watoto yatima Kharkiv.
© UNICEF/Slava Ratynski
Katika kituo cha hifadhi magharibi mwa Ukraine, watoa mafunzo wakilinda watoto kutoka kwa maeneo ya watoto yatima Kharkiv.

Matatizo huongezeka 

Vipaumbele vya mashirika ya Umoja wa Mataifa ni pamoja na kuongeza uwekezaji katika mashirika yasiyo ya kiserikali ya watoa huduma za afya ya akili ili  ya ndani ili kuwasaidia vijana ambao bado wako kwenye matunzo, ili kuunga mkono sera ya serikali ya Ukraine. 

Lakini sio moja kwa moja kutafuta wataalamu wa kutosha kusaidia, "kama wafanyikazi wa kijamii, wanasaikolojia wa watoto na wataalamu wengine wanaathiriwa sawa na mzozo huu", Bwana. Greenberg ameendelea kusema

"Ukianza kufanya hesabu, kuna watoto ambao wanabaki kwenye taasisi ambao hawakuhamishwa ndani au nje, na kuna watoto katika familia za kambo ambao malipo yao yaliingiliwa kwa muda, na kuna watoto kwenye mifumo ya ulezi ambao ni idadi kubwa kwa hivyo unapoweka hili, idadi ya watoto wanaohitaji msaada ambao walikuwa katika mazingira magumu kabla ya mgogoro na ambao udhaifu wao sasa umeongezeka, ni kubwa sana."

Kote nchini Ukrainia, UNICEF ina vitengo 56 vinavyosambaza huduma maalum za afya kwa watoto waliopatwa na kiwewe. Pia kuna timu 12  zinazojitolea mashariki mwa nchi hiyo, ambapo mapigano yanaendelea, Bw. Greenberg amesema. 

"Hadi sasa, timu hizo zinazotembea kutoka sehemu moja hadi nyingine mashariki mwa Ukraine zimefanya kazi kubwa na kushughilkia kesi 7,000 za wanawake na watoto katika suala la kujibu maswali maalum yanayohusiana na unyanyasaji na ripoti ambazo timu hiyo inafuatilia."