Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Burna Boy ziarani Umoja wa Mataifa na kupazia umuhimu wa elimu 

Damini Ebunoluwa Ogulu al maaruf "Burna Boy" (kushoto), mwanamuziki kutoka Nigeria  akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed (kulia) wakati wa ziara yake kwenye makao makuu ya UN. Katikati ni mama mzazi wa Burna Boy, ambaye pia ndiye Meneja wake
UN Video
Damini Ebunoluwa Ogulu al maaruf "Burna Boy" (kushoto), mwanamuziki kutoka Nigeria akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed (kulia) wakati wa ziara yake kwenye makao makuu ya UN. Katikati ni mama mzazi wa Burna Boy, ambaye pia ndiye Meneja wake.

Burna Boy ziarani Umoja wa Mataifa na kupazia umuhimu wa elimu 

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Mwanamuziki nguli na mshindi wa tuzo ya Grammy Burna Boy amezuru makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kwa mwaliko wa Naibu Katibu Mkuu Amina J. Mohammed ambaye pia ni Mnigeria lengo likiwa ni kutumia ushawishi wa mwanamuziki huyo katika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan elimu. 

Kionjo kutoka kwa Burna Boy ndani ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Kulikoni?  

Naibu Katibu Mkuu Amina J.Mohammed anasema “siku hizi mambo si mazuri duniani. Tunahitaji sauti za vijana, sauti zinazowasiliana na idadi kubwa ya vijana wetu duniani kote,” 

Kisha Burna Boy uso kwa uso na mwenyeji wake! 

Bi. Mohammed anasema, “kwa hiyo tunaye Burna Boy mjengoni hii leo. Na ni muhimu sana kwa sababu tunataka kuleta wale walio nje ndani ili wapeleke nje  ujumbe wa Umoja wa Mataifa.” 

Wakiwa ofisini kwa Naibu Katibu Mkuu iliyo ghorofa ya juu kabisa ya jengo alimuonesha Burna Boy aliyeambatanana mama yake ambaye ndio Meneja wake, maeneo mbalimbali maarufu ya jiji la New  York, jengo la Empire State hadi la Chrysler.  

Baada ya hapo ziara kwenye kumbi za mikutano wakianza na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kikao kikiwa kinaendelea, Bi. Mohammed akasema, “wasanii kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu ni washawishi na leo hii ujumbe mmoja kutoka kwa msanini kama Burna Boy, ambaye anagusa nyoyo za watu, anabadili fikra za watu, anazungumzia ukosefu wa haki, ni muhimu kwa malengo haya. Yameundwa yakizingatia haki na matamanio ya watu.” 

Kisha eneo ambako wajumbe wa Baraza la Usalama huzungumza na wanahabari akajulishwa kuwa, “hapa ndipo watu wanazungumza iwe Urusi, Ukraine au Syria au jambo lolote kubwa linalotukabili. Wanakutana na wanahabari. Wanahabari wa kimataifa. 

Damini Ebunoluwa Ogulu al maaruf "Burna Boy"  (kushoto), mwanamuziki kutoka Nigeria  akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed (kulia) wakati wa ziara yake kwenye makao makuu ya UN.
UN /Mark Garten
Damini Ebunoluwa Ogulu al maaruf "Burna Boy" (kushoto), mwanamuziki kutoka Nigeria akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed (kulia) wakati wa ziara yake kwenye makao makuu ya UN.

Ziara ikaendelea kwenye ushoroba wenye zawadi za nchi wanachama kwa Umoja wa Mataifa ikiwemo sanamu ya mwanamke kutoka Nigeria. 

Waliingia ndani ya ukumbi wa Baraza la Usalama kwa kuwa hakukuweko na kikao na baadaye ushoroba wa Bendera za nchi wanachama. 

Kutoka hapo wakaelekea nje yajengo kwenye ushoroba wa miti ya micheri ambayo sasa imechanua…. 

Bi. Mohammed anasema,”napenda kujadili naye kuhusu elimu, kwa sababu elimu ni muhimu sana kwa watu wengi duniani. Inabadilika.” 

Baada ya ziara yake, Burna Boy akasema, . Elimu ndiyo inaamua watoto wetu wa sasa ambao ndio watakuwa viongozi, watakuwa ni watu wa aina gani na watakuwa na fikra zipi. Hivyo jukumu letu leo sisi kuumba fikra hizo, unaelewa, na kuwaweka katika njia sahihi ili historia isijirudie.”