Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN kuzindua ombi la fedha kwa ajili ya operesheni za kibinadamu Ukraine:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akizunugmza na waandishi wa habari jijini New York Marekani. (Maktaba)
UN Photo/Mark Garten)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akizunugmza na waandishi wa habari jijini New York Marekani. (Maktaba)

UN kuzindua ombi la fedha kwa ajili ya operesheni za kibinadamu Ukraine:Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Ukraine Volodymmyr Zelenskyy wa Ukraine na kumhakikishia kuwa Umoja wa Mataifa uko pamoja naye na watu wa taifa lake.

Katika taarifa fupi iliyotolewa na msemaji wake mjini New York Marekani hii leo baada ya mazungumzo hayo Guterres amweleza rais Zelenskyy dhamira ya Umoja wa Mataifa ya kuimarisha msaada wa kibinadamu kwa watu wa Ukraine.

Na katika hilo amemwambia Rais wa Ukraine kwamba “ Jumanne ijayo Umoja wa Mataifa utazindua ombi la fedha kwa ajili ya operesheni zetu za kibinadamu nchini Ukraine.”

Kwa mujibu wa mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa zaidi ya watu 150,000 wamefungasha virago na kuikimbia Ukraine huku idadi hiyo ikirtarajiwa kuongezeka na wengine kwa maelfu wametwanywa katika ameneo mbalimbali ya nchi hiyo. 

Na wote hao Umoja wa Mataifa unasema wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu, ikiwemo maji, malazi, chakula na huduma za afya.