Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wiki ya Malengo ya Dunia wakati wa maonesho ya Expo Dubai 2020 ni muhimu kuonesha ahadi kwa SDGs - Amina J Mohammed

Banda la Al Wasl
Expo 2020 Dubai/Dany Eid
Banda la Al Wasl

Wiki ya Malengo ya Dunia wakati wa maonesho ya Expo Dubai 2020 ni muhimu kuonesha ahadi kwa SDGs - Amina J Mohammed

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed akishiriki katika ufunguzi wa Wiki ya Malengo ya Dunia huko Dubai katika nchi za Falme za Kiarabu au Emarati amesema kuwa tukio hilo ni muhimu ili kuonesha nia na kujitolea kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs.

Wiki hii ya Malengo ya Dunia inawakutanisha watu kutoka nyanja mbalimbali duniani ikifanyika kwa mara ya kwanza nje ya Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York na itaendelea hadi tarehe 21 mwezi huu wa Januari katika maonesho ya Expo Dubai 2020, tukio ambalo lilikuwa lifanyike mwaka 2020 lakini kutokana na janga la coronavirus">COVID-19 lililoikumba dunia mwishoni mwa mwaka 2019 maonesho hayo hayakufayika na yaliahirishwa hadi mwaka jana tarehe 1 Oktoba 2020. Yanatarajiwa kuendelea hadi Machi 31 mwaka 2022. Nchi 192 zinashiriki.  

Jumapili hii, wiki hii ya Malengo ya Kimataifa ambayo imezinduliwa, ni mahususi kwa ajili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu na imekaribisha wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa na viongozi wengine wa dunia kujadili changamoto kama vile ukosefu wa usawa, mabadiliko ya tabianchi na jinsia. 

SDGs 

Warsha hiyo inatoa jukwaa kwa serikali, watunga sera, wafanyabiashara na wananchi kuungana na kufanya kazi kuelekea kuyatimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Mikutano ya namna hiyo itaendelea hadi tarehe 21 ya mwezi huu wa Januari 21. 

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J Mohammed, kuzinduliwa kwa wiki ya Malengo ya Dunia katika Maonesho ya 2020 ya Dubai ni mwanzo wa mwaka wa pili Muongo wa Utekelezaji na kwamba ni fursa muhimu ya kuonesha nia na dhamira inayokua ya kufikia malengo, na kuhakikisha kuwa hakuna anayeachwa nyuma na kupona vyema kutokana na janga la Covid-19. 

Uwezeshaji wa Malengo ya Dunia katika Maonyesho ya Dubai 2020
Expo 2020 Dubai/Christopher Edralin
Uwezeshaji wa Malengo ya Dunia katika Maonyesho ya Dubai 2020

 

Agenda 2030 

Malengo ya Maendeleo Endelevu, ambayo ni sehemu ya Ajenda ya mwaka 2030, yalipitishwa na Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015 na yanatoa mpango wa pamoja wa amani na ustawi kwa watu na sayari, sasa na katika siku zijazo. 

Kuna malengo 17 ambayo pamoja na mambo mengi, yanalenga kuboresha afya na elimu, kupunguza ukosefu wa usawa na kuchochea ukuaji wa uchumi. Wakati huo huo, malengo yanashughulikia mabadiliko ya tabianchi na kufanya kazi kuhifadhi bahari na misitu yetu. 

Umoja wa Mataifa 

Umoja wa Mataifa umetayarisha mfululizo wa matukio wakati wa Maonesho ya Dubai 2020 katika nafasi iliyojitolea kuelezea jukumu la Umoja huo na Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. 

Umoja wa Mataifa ukilenga kueleza kwa kina jinsi unavyofanya kazi ili kudhibiti changamoto za kimataifa, umeandaa maonesho ya "Mission Possible" kuonesha “Inawezekana”

Banda hili katika maonesho ya Dubai, Dubai Expo 2020 limepatiwa jina banda la fursa. Kila jambo linawezekana.
Expo 2020 Dubai/Suneesh Sudhakaran
Banda hili katika maonesho ya Dubai, Dubai Expo 2020 limepatiwa jina banda la fursa. Kila jambo linawezekana.

 

Banda la Umoja wa Mataifa linawaleta pamoja maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa na watu wengine wenye ushawishi, pamoja na viongozi wengine kutoka nyanja na maeneo mbalimbali  ili kuzungumza kuhusu masuluhisho ya kibunifu na mipango inayoshughulikia Malengo ya Kimataifa kama vile ukosefu wa usawa, mabadiliko ya tabianchi na ukosefu wa usawa wa kijinsia. 

Matukio yote yanayoendelea pamoja na ratiba kamili, vinapatikana katika wavuti rasmi wa Expo Dubai 2020.