Umoja wa Mataifa walaani mauaji nchini Nigeria

10 Januari 2022

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mashambulizi ya kutisha yaliyotekelezwa mwishoni mwa juma katika Jimbo la Zamfara nchini Nigeria ambapo raia wengi waliuawa.

Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizofiwa kwenye shambulio hilo.

Katibu Mkuu pia amezitaka mamlaka za Nigeria kuhakikisha zinafanya juhudi zote ili kuwapata na kuwafikisha mahakamani wale wote waliohusika na uhalifu huo mbaya.

Umoja wa Mataifa inaunga mkono na kuonesha mshikamano na serikali ya Nigeria katika mapambano na vita dhidi ya ugaidi, itikadi kali za kikatili na uhalifu uliopangwa.

 

 

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter