Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UN alaani mauaji ya watu 8 nchini Iraq

Wasichana wa Kikurdi wanarejea nyumbani kutoka shuleni katika mji wa Dohuk katika Mkoa wa Kurdistan kaskazini, Iraq. (Maktaba)
© UNICEF/M© UNICEF/Michael Kamber
Wasichana wa Kikurdi wanarejea nyumbani kutoka shuleni katika mji wa Dohuk katika Mkoa wa Kurdistan kaskazini, Iraq. (Maktaba)

Katibu Mkuu wa UN alaani mauaji ya watu 8 nchini Iraq

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani shambulio la risasi lililotokea jana huko Zakho jimboni Dohuk katika mkoa wa Kurdish nchini Iraq na kusababisha vifo vya watu nane na wengine 23 kujeruhiwa. 

Taarifa ya Naibu Msemaji wa katibu Mkuu Farhan Haq aliyoitoa leo jijini New York, Marekani imesema “Katibu Mkuu anatoa wito wa kufanyika haraka kwa uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo ili kubaini mazingira ya tukio hilo na kuhakikisha kuna uwajibikaji.”

Haq pia amesema Katibu Mkuu ametuma salama za pole kwa familia zilizoathirika na tukio hilo na kuwatakia ahueni wagonjwa wote wapone kwa haraka.