Skip to main content

Arctic yavunja rekodi ya kufikia nyuzi joto 38℃ kwingine kutafuata nyayo:WMO

mvuvi anajaribu kuzuia wavu wake kuvutwa chini na kilima cha barafu katika bahari ya Greenland.
Climate Visuals Countdown/Turpin Samuel
mvuvi anajaribu kuzuia wavu wake kuvutwa chini na kilima cha barafu katika bahari ya Greenland.

Arctic yavunja rekodi ya kufikia nyuzi joto 38℃ kwingine kutafuata nyayo:WMO

Tabianchi na mazingira

Rekodi mpya ya ya kutia hofu ya ongezeko la joto katika eneo la Arctic ya  nyuzi joto 38C, au zaidi kidogo ya nyuzi joto 100 vipimo vya Fahrenheit, ilithibitishwa leo na shirika la hali ya hewa duniani WMO. 

Kwa mujibu wa shirika hilo cha kusikitisha ni kwamba, viwango wa hali ya joto vilivyorekodiwa mwezi Juni mwaka jana katika mji wa Siberia wa Verkhoyansk - ulioko kilomita 115 kaskazini mwa mzunguko wa Arctic ni "moja tu ya mfululizo wa uchunguzi wa unaoweza kuvunja rekodi ya joto kutoka duniani kote kwa mwaka wa 2020, hali ambayo WMO inataka kuithibitisha. 

"WMO asubuhi ya leo limebaini joto la nyuzi 38C ambalo ni sawa na nyuzi 100.4F katika mji wa Verkhoyansk nchini Urusi," msemaji wa WMO Clare Nullis amewaambia waandishi wa habari huko Geneva Uswis na kuongeza kuwa kiwango hicho "Kilirekodiwa tarehe 20 Juni 2020 na tumetkibaini kuwa ni cha rekodi mpya ya Arctic." 

Likielezea halijoto kama inafaa zaidi bahari ya Mediterania kuliko Arctic, WMO imesema katika taarifa kwamba wastani wa halijoto katika eneo la Arctic la Siberia ilifikia nyuzijoto 10C juu ya kiwango cha kawaida kwa muda mrefu wa majira yaliyopita ya kiangazi. 

Miezi mibaya zaidi ya majira ya joto  

"Ukirudisha akili yako mwaka jana, utakumbuka kulikuwa na wimbi la joto Siberia la kipekee na la muda mrefu, na matokeo ya wimbi hili la joto tulishuhudia moto mbaya wa nyika na uliosambaa sana huko Siberia na tuliona upoteve mkubwa wa barafu katika bahari ya Arctic mwishoni mwa msimu wa kiangazi,” amesema Bi. Nullis. 

Hali kama vile tanuru pia ilichangia 2020 kuwa moja ya miaka mitatu ya joto zaidi katika rekodi ya dunia, msemaji huyo wa WMO ameelezea, akiongeza kuwa wimbi la joto la Siberia "lingekuwa jambo lisilowezekana bila mabadiliko ya tabianchi". 

Kwa kukabiliana na rekodi ya wimbi lhilo a joto la Arctic, shirika hilo la hali ya hewa la Umoja wa Mataifa limeunda kitengo kipya cha viwango vya joto vinavyorekodiwa.  

Katika Kumbukumbu ya WMO ya hali ya hewa na hali ya hewa Iliyokithiri, aina mpya ya rekodi ya joto imeorodheshwa kama "joto la juu zaidi lililorekodiwa katika eneo au kaskazini mwa mzunguko wa Arctic la nyuzi 66.5⁰.” 

Barafu iliyoko katika Bahari huko Uruguay Bay, Kisiwa cha Laurie, Orkney Kusini, Antarctica
WMO/Diego Ferrer
Barafu iliyoko katika Bahari huko Uruguay Bay, Kisiwa cha Laurie, Orkney Kusini, Antarctica

Joto linaongezeka kwa akasi arctic 

Wakati WMO imeonya mara kwa mara kwamba Arctic ni moja ya sehemu ambako joto linazoongezeka kwa kasi duniani, "Linaongezeka zaidi ya mara mbili ya wastani wa kimataifa", amesema Bi. Nullis na kusisitiza kuwa mabadiliko ya tabianchi pia yameongeza joto mahali pengine, ambako shirika la Umoja wa Mataiifa linafuatilia na kuthibitisha. 

Hii ni pamoja na kiwango kipya cha juu cha joto katika bara la Antarctic cha nyuzi joto 18.3C ambacho kilirekodiwa katika ukingo wa Argentina, Esperanza. 

Wachunguzi wa WMO pia wanatafuta kuthibitisha viwango vya joto vya nyuzi joto 54.4C vilivyorekodiwa mwaka wa 2020 na 2021 katika sehemu yenye joto zaidi duniani, za Death Valley huko California nchini Marekani. 

Kwa kuongezea, Bi. Nullis amesema pia wanatathmini rekodi mpya ya joto ya Ulaya ya nyuzi joto 48.8C katika kisiwa cha Italia cha Sicily wakati wa msimu huu wa majira ya joto. 

"Kumbukumbu ya WMO ya hali ya hewa na hali ya hewa Iliyokithiri haijawahi kuwa na uchunguzi mwingi unaoendelea kwa wakati mmoja, kama sasa" Katibu Mkuu wa WMO Petteri Taalas, amesema katika taarifa yake.