Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatangaza leseni ya wazi ya utafiti wa kupamba na COVID-19

Mwanasayansi akipima sampuli za COVID-19 katika maabara nchini Sierra Leone.
WHO
Mwanasayansi akipima sampuli za COVID-19 katika maabara nchini Sierra Leone.

WHO yatangaza leseni ya wazi ya utafiti wa kupamba na COVID-19

Afya

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na lile la hati miliki za dawa MPP hii leo wametangaza leseni ya kwanza ya uwazi ya kimataifa ya teknolojia inayohusiana na COVID-19 iliyotolewa na baraza la kitaifa la utafiti la Hispania CSIC.

Akitangaza habari hiyo njema kutokea Geneva Uswisi Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Ghebreyesus amesema leseni hiyo inatoa ruhusa kwa nchi zote kutumia matokeo ya utafiti uliofanywa na Baraza la utafiti la Hispania CSIC.

Matokeo ya utafiti wa CSIC yamekuja na mbinu zinazoweza kututumika nchi yeyote ulimwenguni kukagua vyema namna kingamwili zinavyoweza kupambana na virusi vya coronavirus">COVID-19 , maambukizi ya Corona au chanjo.

Dkt. Tedros ameishukuru serikali ya Hispania na baraza lake. "Ninaipongeza sana CSIC, taasisi ya utafiti wa umma, kwa kujitolea kwake kwa mshikamano na kutoa ufikiaji wa teknolojia na ujuzi wao ulimwenguni. Hii ni aina ya leseni ya uwazi tunayohitaji kukabiliana na janga hili. Ninawasihi watengenezaji wa chanjo, matibabu na uchunguzi wa COVID-19 kuiga mfano huu.”

Utafiti huu unaweza kutumika hata kwenye miundombinu hafifu hasa vijijini katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

Miongoni mwa waliofurahishwa na kutolewa kwa leseni hii ni Rais wa Costa Rica ambaye ameipongeza serikali ya Hispania na baraza lake na kueleza mbinu hiyo iliyotolewa na wanasayansi watafiti itasaidia kushindana na hali ya sasa ya janga la Corona

"Leseni hii ni ushuhuda wa kile tunachoweza kufikia tunapoweka watu mbele wakati huu tukiwa katikati ya juhudi zetu za kimataifa na kimataifa. Inaonesha kwamba mshikamano na ufikiaji sawa unaweza kupatikana na ni vyema kuendelea kuunga mkono kanuni za uwazi, ushirikishwaji na kutojitenga." Amesema " Carlos Alvarado Quesada, Rais wa Costa Rica

Shirika la hati miliki za Dawa MPP nalo limetoa wito kwa makampuni na watafiti wengine duniani kujitokeza na kutoa leseni zenye uwazi ili kuwezesha tafiti walizozifanya kusaidia watu wote duniani kwa unafuu.