Naibu Katibu Mkuu wa UN na serikali ya Kenya wajadili ushirikiano, COVID-19 na usalama

11 Septemba 2021

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed yuko ziarani Afrika Mashariki ambapo akiwa nchini Kenya amepata fursa ya kuzungumza na viongozi wa serikali ya nchi hiyo. 

Kabla ya kuelekea Ikulu mjini Nairobi kukutana na Rais Uhuru Kenya, Bi. Mohammed alikutana na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Raychelle Omamo na kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo hospitali ya corona au COVID-19 ambayo ilionekana kuwa kama ndoto wakati ilipopendekezwa na kwa sasa Kenya ina furaha kubwa kusema ndoto hiyo inatimia. 

Masula mengine waliyogusia ni pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya serikali ya Kenya na Umoja wa Mataifa. 
Na kabla ya kuondoka kuelekea Tanzania ambako ndiko kituo cha pili cha ziara yake Naibu Katibu Mkuu huo alielekea Ikulu jijini Nairobi kufanya mazungumzio na Rais Uhuru Kenyata. 

Pamoja na mambo mengine wawili hao wamejadili masuala yeye umuhimu mkubwa kwa Kenya na Umoja wa Mataifa haswa suala la amani na usalama wa kikanda, hatua zinazochukuliwa na serikali kupambana na janga la COVID-19 na maandalizi ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP26 unaotarajiwa kufanyika Scotland baadaye mwaka huu. 

Bi. Mohammed katika safari yake ya Ikulu ya Nairobi aliambatana na mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Kenya UNOG, Zainab Bangura na mratibu mkazi wa Umoja wa Masaifa ncnhini Kenya Stephen Jackson. 

Nchini Tanzania Bi. Mohammed anatarajiwa mbali ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kukutana pia na viongozi wa serikali na kujadili masuala mbalimbali. 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter