Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima tushikamane kujumuisha wenye ulemavu:Mohammed

Binti mwenye mika 9 akicheza kwenye eneo jumuishi la michezo katika shule yake kwenye kambi ya wakimbizi ya Za'atari nchini Jordan
© UNICEF/Christopher Herwig
Binti mwenye mika 9 akicheza kwenye eneo jumuishi la michezo katika shule yake kwenye kambi ya wakimbizi ya Za'atari nchini Jordan

Lazima tushikamane kujumuisha wenye ulemavu:Mohammed

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Jumuiya ya kimataifa imeafikiana mfumo wa kusongesha mbele haki za watu wenye ulemavu ikiwemo katika Nyanja ya maendeleo, lakini bado kuna mapengo mengi baina ya azma hii na hali halisi inayowakabili kila siku mamilioni ya watu wenye ulemavu amesema naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed.

Akizungumza hii leo Jumamosi kwenye mkutano wa kimataifa mjini Doha Qatar amesema ukiwa na wanachama 181,mkataba wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu ni miongoni mwa mikaba iliyoridhiwa nan chi nyingi duniani na ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 inaweka ahadi muhimu ya kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu hawaachwi nyuma katika lengo la kimataifa la kwa ajili ya amani na ustawi kwenye dunia yenye afya.

Naibu Katibu Mkuu ameongeza kuwa “lakini mapengo bado yapo baina ya hatua hizi za hamasa na hali halisi ya Maisha yanayowakabili takribani watu bilioni moja wenye ulemavu duniani , takribani asilimia 80 kati yao wakiishi katika nchi zinazoendelea ambako ni miongoni mwa makundi ynayotengwa katika kila janga linaloathiri jamii.”

Vikwazo bado vipo na unyanyapaa ukichochea ubaguzi

Bi Mohammed katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo wa Doha wa kimataifa kuhusu ulemavu na maendeleo amesema “idadi ya watu wenye ulemavu wanaoishi katika umasikini na njaa ni kubwa kuliko na katika baadhi ya nchi ni mara mbili ya watu wengine na kwamba kaulimbiu ya watu wenye ulemavu ni hakuna chochote kuhusu sisi, bila sisi,hii inapaswa kuwa kweli sio tuu kwa jinsi Umoja wa Mataifa unavyojiuhusisha na asasi za kiraia bali katika maeneo yote ya kazi zetu hasa tunapojitahidi kutimiza ahadi ya mkakati wa ujumuishaji watu wenye ulemavu ”

Amehimiza kwamba ukilinganisha na watu wengine, watu wenye ulemavu wanakabiliwa na vikwazo vingi wanaposaka fursa za afya. “kimataifa idadi ya watu wenye ulemavu walioajiriwa ni nusua ya wale wasio na ulemavu” na kwamba ndio walio katikahatari Zaidi ya kutohudhuria shule na kumaliza elimu ya msingi.

Ameongeza kuwa katika kanda zote unyanyapaa unaowakabili watu wenye ulemavu unaendelea na unachangiwa na kutokuelewa haki zao na tahamani ya mchango wao katika jamii”

Bi. Mohammed amesisitiza kwamba kuendelea kwa unyanyapaa huo kunachochea ubaguzi na kufanya watu wenye ulemavu kunyimwa fursa sawa za elimu, ajira, huduma za afya na fursa za kushiriki maisha katika jamii. “Na kwa watu wengi  wenye ulemavu hususan wanawake na wasichana ubaguzini mara dufu.”

Hatua zaidi zahitajika kubadili hali hii

Naibu Katibu Mkuu amesisitiza kwamba “Hali hii haiwei kuendelea na haikubaliki. Inakwenda kinyume na wajibu na ahadi yetu ya pamoja ya utu, wajibu wetu chini ya sheria zakimataifa na suala muhimu la ujumuishaji wa watu wenye ulemavu. Ni juu yetu, viongozi kutoka serikalini,makampuni ya biashara, asasi za kiraia , mashirika ya watu wenye ulemavu,mashirika ya kimataifa na wadau wengine kubadili hali hii.”

Mapema Bi.Mohammed alipongeza kazi kubwa ya bila kuchoka inayofanywa na mwana mfalme Sheikha Moza bint Nasser ambaye amemuelezea kama mmoja wa watu waliojitolea sana  na wanaharakati waliopo katika kuboresha elimu kote duniani na kuhakikisha kwamba hakuna anayebaki nyuma hususan watu wenye ulemavu. Amesema ni muhimu sana “kuongeza juhudi zetu za pamoja kuhusu kujumuisha watu wenye ulemavu katika kutimiza SDGs.”

Mambo ya kuyafanyia kazi

Ametaja maeneo manne ya kuchukua hatua ambayo ni lazima  na kusema maeneo hayo katika baadhi ya nchi zinahitaji kuongeza nguvu ni katika upatikanaji wa takwimu za wakati na zinazoaminika, pili amesema rasilimali ni muhimu sana  nan chi zinapaswa kufanya suala la wenye ulemavu kuwa ni kipaumbele katika bajeti zao za kitaifa.

Tatu amesema ni suala la kuboresha fursa ambazo amesema ni lazima katika kuhakikisha ujumuishwaji na ushiriki wa kikamilifu wa watu wenye ulemavu katikajamii.

Na nne na mwisho ametaka kuwe na msaada kwa watu wenye ulemavu hasa katika maeneo yenye mizozo na changamoto za kibinadamu.