Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Nchini Yemen mama wa mtoto wa miezi 18 amempeleka kupatiwa huduma ya utapiamlo

Mustakbali wa Yemen uko njiapanda aonya mratibu mwandamizi wa misaada wa UN

© UNICEF/Saleh Hayyan
Nchini Yemen mama wa mtoto wa miezi 18 amempeleka kupatiwa huduma ya utapiamlo

Mustakbali wa Yemen uko njiapanda aonya mratibu mwandamizi wa misaada wa UN

Amani na Usalama

Mizozo na vurugu zinazoendelea nchini Yemen zinaendelea kuathiri sana watu wa nchi hiyo ambao wanahitaji kwa kila hali mapigano kumalizika, ili waweze kujenga maisha yao, amesema leo afisa mkuu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataif nchini humo. 

“Nimeona uharibifu wa shule, viwanda, barabara na madaraja; Nimeona uharibifu wa mifumo ya umeme kwa hivyo ni nini kilichofanya Yemen ifanye kazi miaka saba iliyopita kwa visa vingi ambavyo havipo tena ", amehoji David Gressly, mratibu wa mkazi na misaada ya kibinadamu nchini Yemen. 

Akiongea mjini Geneva Uswisi baada ya mwishoni mwa juma, gari lililosheheni bomu kulipuka kwenye uwanja wa ndege wa Aden na kuwaacha watu 25 wamekufa na kujeruhi wengine 110, mfanyikazi huyo wa zamani wa misaada ameonya juu ya kuongezeka kwa mapigano katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Marib. 
Mapigano yanaziba fursa 
 
"Hali hii sasa inaongeza idadi ya watu kuhama zaidi katika eneo hilo, mahali ambapo tayari tuna zaidi ya watu milioni moja waliokimbia makazi yao. Na pili, tuna maeneo ambapo mapigano yanaendelea na hatuwezi kutoa msaada". 

Bwana Greassly amesema wasiwasi wa muda mrefu juu ya uwezekano wa njaa nchini humo ulichochea ombi lililoongozwa na Umoja wa Mataifa la dola bilioni 3.6 bilioni kwa ajili ya ufadhili, na tangu mwezi Machi wameweza kukusanya karibu dola bilioni $ 2.1 hadi sasa. 

Dola zingine za ziada milioni 500- $ 600 pia ziliahidiwa wakati wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa wa hivi karibuni, ameongeza Bwana Gressly akibainisha kwamba hatua za kimataifa zimekuwa kubwa zaidi kuliko dharura zingine, "imekuwa ikilenga sana  na tunaelewa kwanini suala la uhakika wa chakula na upande wa lishe, kwa hatua za kuokoa maisha mara moja ”.

Hali tete 

Gressly amesisitiza kuwa hii imeacha hali ndani ya Yemen kuwa dhaifu sana na na hali itakuwa mbaya zaidi endapo  hatutopata ahadi mpya kwa wakati kwa ajili yam waka 2022,na hali itarejea kule tulikokuwa Machi. 

Ameelezea kuwa watu walihitaji zaidi ya huduma ya dharura: “Afya, elimu, maji, ufikiaji wa huduma za msingi na msaada kwa wakimbizi wa IDP na msaada wa kujikimu kimaisha, ombi hilo linafadhiliwa chini ya asilimia 20, na kwa hivyo wakati kuokoa maisha ni muhimu, hatuwezi, hatuwezi kupuuza mengine ". 

Watumishi wa umma wanahitaji msaada 

Kitu muhimu kwa ajili ya Yemen kuweza kujikwamua ni msaada kwa wafanyikazi wa serikali wa nchi hiyo, ambao wengi wao hawajalipwa kwa miezi mingi, wakati wa mzozo kati ya serikali ya Abd Rabbo Mansour inayoungwa mkono kimataifa na vikosi vya upinzani vya Houthi, ambavyo vinadhibiti sehemu kubwa ya kaskazini mwa nchi. 

Bwana Gressly amesisitiza umuhimu wa kutafuta njia za kuwasaidia hawa wafanyikazi wa serikali kwani ni muhimu kwa nchi kupata kujikwamua na mipango ya misaada ya Umoja wa Mataifa. Bila wao, "Hatua zote za kibinadamu" zina hatari ya kuwa ghali zaidi.”