Ingawa mgogoro umeepukwa mizizi ya kutokuwa na uhakika wa chakula Malawi lazima ikatwe:OCHA

2 Machi 2019

Baada ya ziara ya siku mbili nchini Malawi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA, Mark Lowcok amesema leo Jumamosi kwamba mgogoro wa chakula nchini humo umeepukwa asante kwa misaada ya kibinadamu iliyotolewa na mvua kubwa iliyonyesha, lakini metoa wito wa hatua madhubuti kuchukuliwa ili kushughulikia miziz ya kutokuwepo kwa uhakika wa chakula inayoathiri mara kwa mara taifa hilo.

Katika taarifa yake iliyotolewa mjini Lilongwe mji mkuu wa Malawi mkuu huyo wa OCHA amesema kukiwa kumeepukwa janga la uhakika wa chakula hivi sasa ni rahisi kushawishika kujisahau kuendelea na juhudi lakini hatua zinahitajika kushughulikia mizizi ya tatizo hili la kutokuwa na uhakika wa chakula nchini Malawi kwa kupanua wigo wa aina ya uchumi wa kilimo, kuweka sera rafiki za soko la kilimo, kujenga mnepo wa kukabili mabadiliko ya tabianchi na ukame unaojirudia mara kwa mara na kuimarisha mifumo inayolinda jamii kutokana na janga hili  suala ambalo ni kipaumbele.

Pia ameongeza kuwa ni muhimu kuendelea kutoa msaada wa kibinadamu katika kipindi chote cha muambo ili kuwapa fursa wale waliokuwa katika hali mbaya na wasiojiweza kuweza kurejea tena katika hali ya kawaida.

Baada ya matarajio ya utabiri wa mwishoni mwa mwaka jana kwamba watu milioni 3.3 hawatokuwa na uhakika wa chakula Malawi kati ya Januari na Machi , Lowcock alitoa dola milioni 10 kutoka fuko la dharura la Umoja wa Mataifa CERF ili kuisaidia nchi hiyo kuepuka janga la kibinadamu la chakula.

Wanawake na wasichana ndui walio hatarini zaidi

Mratibu huyo wa OCHA amezuru eneo la Salima ili kushuhudia miradi inayofadhiliwa na fedha hizo za CERF inavyosaidia hasa katika masuala ya maji, usafi na huduma za afya.

Kwa msaada wa fedha hizo amesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP, shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF , shirika la afya duniani WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA wataweza kuwasaidia watu zaidi ya 683,000 katika wilaya tisa katika kipindi cha miezi sita.

Lowcok ameongeza kuwa “Msaada huo wa CERF unalenga zaidi wanawake na watoto ambao tunatambua ndio wanakuwa waathirika wakubwa katika wakatu wa kutokuwepo kwa uhakika wa chakula. Nimekutana na wanawake ambao hawakuweza kulisha watoto wao lakini sasa wanaweza pia wanaweza kuwapeleka shuleni kusoma wakiwa wameshiba kutokana na msaada huu.”

Mballi ya mahindi yaliyotolewa na serikali mashirika ya misaada yamegawa fedha kwa wilaya zilizoathirika zaidi na kusaidia matibabu ya utapiamlo uliokithiri hususan miongoni mwa watoto.

Makadirio ya hivi karibuni yanaashiria kwamba uzalishaji wa chakula kwa mwaka 2019 utakuwa bora zaidi ya mwaka jana. Lakini Malawi inakabiliwa na msimu wa muambo ambao kwa kawaida huanza Oktoba hadi April ambapo mamilioni ya watu nchini humo wako katika tishio kubwa la kuongezeka hali ya kutokuwa na uhakika wa chakula.

Bofya hapa kutoa maoni yako kuhusu vipindi vyetu:https://www.surveymonkey.com/r/JGDD2PZ

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter