Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili mpya kwa ajili ya Yemen umetutia moyo:WFP

Wafanyakazi wakipanga msaada wa chakula katika nyumba ya hifadhi Lahj, Yemen. (Julai 1 2019)
WFP/Saleh Baholis
Wafanyakazi wakipanga msaada wa chakula katika nyumba ya hifadhi Lahj, Yemen. (Julai 1 2019)

Ufadhili mpya kwa ajili ya Yemen umetutia moyo:WFP

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema limetiwa moyo na tarifa za ufadhili mpya kwa ajili ya Yemen ingawa bado taifa hilo linakabiliwa na pengo kubwa la fedha kwa ajili ya huduma za kibinadamu.

Kupitia taarifa ya shirika hilo iliyotolewa leo mjini Geneva Uswis, mkuu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Mark Lowcoc ametangaza kuhusu fufadhili huo ambao amesema fedha zitatolewa hivi karibuni kushughulikia mahitaji ya dharura kwa maelfu ya watu wa Yemen.

WFP inakabiliwa na pengo kubwa la fecha na bila msaada wa haraka wa feha shirika hilo litalazimika kupunguza mgao wa chakula kwa mamilioni ya watu wa Yemen kuanzia mwezi Oktoba.

Tunahitaji haraka dola milioni 600 ili kuweza kuendesha operesheni zetu yemen kwa miezi sita ijayo” amesema Herve Verhoosel msemaji wa WFP na kuongeza kwamba Tuna miezi mitatu tu au minne ya kuweza kuingiza na kusafirisha chakula cha kutosha kulisha mamilioni ya watu Yemen ambao wanaishi kwa kutegemea msaada wa WFP.Tiunahitaji kuendelea kuwa na bidhaa zinazoingia Yemen kila wakati il;I kuhakikisha kwamba kila mwezi tunapata chakula cha kutosha kwa ajili ya watu wasiojiweza. Mahitaji ya WFP kwa mwezi ni takribani dola milioni 200 wakati huu ambapo tunaendelea kuongeza operesheni zetu ili kuwafikia watu milioni 12 kila mwezi.”

Tangu mwezi Mei hadi Julai WFP imefanikiwa kuwafikia watu zaidi ya milioni 11 kila mwezi ikiwapa msaada wa chakula. Mgao wa mwezi Agosti umekamilika kwa sababu mgao huanza katikati ya mwezi hadi katikati ya mwezi mwingine.  WFP imesisitiza kuwa jumuiya ya misaada ya kibinadamu haiwezi kupunguza kasi ya msaada sasa kwani utratibu mmzuri wa misaada ya jumuiya hiyo umesaidia kuepusha zahma kubwa ya kibinadamu Yemen, lakini endapo huduma hizi zinasita au kutofanikiwa basi hali itaanza kuzorota tena.

Vita nchini Yemen vinasalia kuwa chachu kubwa ya kutokuwa na uhakika wa chakula ambapo watu milioni 22 sawa na asilimia 70 ya watu wote nchini humo hawana uhakika wa chakula.