Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Posta ina mchango mkubwa kwa jamii na uchumi wetu:UN

Shirika la posta duniani, UPU linazindua awamu ya pili ya kushirikiana na mashirika 8 ya posta duniani kuchagiza huduma za ujumiushwa wa fedha kimtandao katika mataifa 8.
UPU
Shirika la posta duniani, UPU linazindua awamu ya pili ya kushirikiana na mashirika 8 ya posta duniani kuchagiza huduma za ujumiushwa wa fedha kimtandao katika mataifa 8.

Posta ina mchango mkubwa kwa jamii na uchumi wetu:UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Leo ni siku ya posta duniani na katika siku hii tunatambua mchango mkubwa na muhimu wa wahudumu wa posta kwa jamii zetu na uchumi wetu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Kupitia ujumbe wake maalum wa siku hii inayoadhiumishwa kila mwaka Oktoba 9, Antoniuo Guterres amesema “Mamilioni ya wahudumu wa posta wasafirisha mabilioni ya barua na vifurishi kupitia maelfu kwa maelfu ya ofisi za posta kote duniani na hivyo kuzihudumia na kuziunganisha jamii kote duniani.”

Maudhui ya siku yam waka huu ni “ubunifu kwa ajili yua kujikwamua vyema” na siku hii inaadhimishwa katika siku ya kumbukumbu ya kuanzishwa kwa muungano wa posta duniani UPU mwaka 1874 kwenye mji mkuu wa Uswis Bern.

Kuhusu kaulimbiu ya mwaka huu UPU inasema “Wakati janga la corona au COVID-19 lilipozuka na kuathiri nchi zote duniani ikiwemo miundombinu ya mifumo iliyopo ya usafirishaji posta bado ilitafuta njia ya kuendelea kutoa huduma kwa jamii. Na ni kwa ubunifu huu wa post ana mnepo wake wa kutaka kuhudumia jamii ndio unaosherehekewa katika siku ya posta duniani.”

Kuchambua barua
Universal Postal Union
Kuchambua barua

Siku ya posta duniani ilitangazwa rasmi na bunge la UPU lililofanyika Tokyo Japan mwaka 1969.

Na tangu wakati huo kote duniani watu wanasherehekea siku ya Posta. Na posta katika nchi nyingi duniani hutumia siku hii kuzindua na kuchagiza huduma na bidhaa mpya za posta.

Mwaka 2015 nchi zote duniani zilizahidi kushirikiana kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDG’s ambayo yanalenga kutokomeza umasikini na njaa, pengo la usawa na haki, na kuchukua hatua za kubadili mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi.

Ikitimiza sehemu yake katika juhudi hizo za kimataifa posta leo hii inajukumu kuliko wakati mwingine wowote kwa kutoa miundombinu kwa ajili ya maendeleo.