COVID-19, mabadiliko ya tabianchi ni mwiba wa maendeleo mijini- UN

4 Oktoba 2021

Katika maadhimisho siku ya makazi duniani, ambayo mwaka huu ina kaulimbiu "Kuongeza kasi ya hatua mijini ili kuwa na dunia isio na hewa ukaa", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kufanya kazi pamoja "ili kutumia uwezo wa mabadiliko kwa ajili ya hatua endelevu mijini".

Kila mwaka Oktoba 4, Umoja wa Mataifa unasherehekea siku ya makaazi duniani na mwaka huu sherehe zinaambatana na mfululizo wa midahalo ya moja kwa moja na mtandaoni, iliyoandaliwa huko Yaoundé, Kamerun.

Kaulimbiu yam waka huu ni "Kuongeza kasi ya hatua mjini ilikuwa na dunia isiyo na hewa ukaa " inakusudia kujikita na majadiliano ya juu ya upatikanaji wa nyumba na umuhimu wa kuunda miji kwa siku zijazo.

Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa siku hii, pamoja wa  watataalam wengine kadhaa umejikita na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa makazi kote ulimwenguni, ili kusisitiza hofu hiyo.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu António Guterres, katikati ya karne, hii "zaidi ya wakazi bilioni 1.6 wa mijini wanaishi kwa kuvumilia joto la juu la nyuzi joto 35 kwa wastani wakati wa majira ya joto".

Asubuhi katika mitaa ya Melen, mtaa wa mabanda katikati ya mji mkuu wa Cameroon, Yaoundé. Kwa muda mrefu Cameroon imekuwa katika mgogoro wa ndani.
UN-Habitat/Kirsten Milhahn
Asubuhi katika mitaa ya Melen, mtaa wa mabanda katikati ya mji mkuu wa Cameroon, Yaoundé. Kwa muda mrefu Cameroon imekuwa katika mgogoro wa ndani.

Ongezeko la idadi ya watu wa mijini

Kufikia mwaka 2050, Umoja wa Mataifa unakadiri idadi ya watu mijini kuongezeka kwa nusu, ambapo leo hii idadi ya watu duniani ni karibu bilioni 4.5. Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasisitiza kuwa robo tatu ya miundombinu muhimu italazimika kujengwa kwa miaka 30 ijayo.

Wakati dunia inajikwamua kutoka janga la COVID-19 , Bwana Guterres anaamini kuwa mipango ya kuchochea uchumi "Inatoa fursa ya kuweka hatua za mabadiliko ya tabianchi, nishati mbadala na maendeleo endelevu katikati ya mikakati na seraza miji".

Mkuu wa Umoja wa Mataifa ataka kazi ya pamoja "kutumia uwezekano wa mabadiliko ya hatua endelevu za mijini, kwa faida ya sayari dunia na watu".

Umoja wa Mataifa umeitenga Jumatatu ya kwanza ya mwezo Oktoba ya kila mwaka kuwa “Siku ya Makazi Duniani” kutafakari juu ya hali ya makazi na haki ya kimsingi ya kila mtu ya makazi.

Kupitia sherehe hii, Umoja wa Mataifa pia unakusudia kuukumbusha ulimwengu kuwa kila mtu anawajibika kwa mustakabali wa makazi ya wanadamu.

Mji wa London, Uingereza
Unsplash/Ali Yaqub
Mji wa London, Uingereza

 

 

TAGS: Siku za UN, Siku ya Makazi, UN-HABITAT, COVID-19

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter