COVID-19, mabadiliko ya tabianchi ni mwiba wa maendeleo mijini- UN
Katika maadhimisho siku ya makazi duniani, ambayo mwaka huu ina kaulimbiu "Kuongeza kasi ya hatua mijini ili kuwa na dunia isio na hewa ukaa", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kufanya kazi pamoja "ili kutumia uwezo wa mabadiliko kwa ajili ya hatua endelevu mijini".