Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatangaza mlipuko wa Ebola Corte D'Voire

Cote d'Ivoire imetangaza mlipuko wa Ebola baada ya miaka zaidi ya 25
WHO
Cote d'Ivoire imetangaza mlipuko wa Ebola baada ya miaka zaidi ya 25

WHO yatangaza mlipuko wa Ebola Corte D'Voire

Afya

•    Mgonjwa alitokea nchini Guinea
•    Chanjo zapelekwa kukinga maambukizi 
•    WHO imesema hakuna haja ya kufunga mji wa Abijan alipolazwa mgonjwa.

Mgonjwa wa kwanza wa Ebola amegundulika nchini Corte D'Voire shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni limetangaza rasmi hii leo baada ya kupokea taarifa kutoka wizara ya afya ya nchini Corte D'Voire ikiwa ni zaidi ya miaka 25 tangu kutoweka ugonjwa huo nchini humo mwaka 1994. 

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Dkt.Matshidiso Moeti amesema mgonjwa huyo aliyetokea nchini Guinea amelazwa mjini Abijani baada ya kufanyiwa uchunguzi na taasisi ya Pasteur na kuthibitika kuwa na Ebola.

Guinea ilikumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kwa muda wa miezi 4 ambapo ulitangazwa kuisha rasmi 19 Juni 2021 hata hivyo Dkt. Moeti amesema “Hakuna dalili zinazoonesha mgonjwa huyu wa sasa nchini Corte D’Voire anahusishwa na mlipuko uliotokea nchini Guinea. Uchunguzi na upimaji zaidi unaendelea kubaini iwapo kuna uhusiano wowote wa milipuko hii miwili.”


  Kuhusu mgonjwa 

Uchunguzi wa awali umebaini mgonjwa alisafiri kwa barabara kutokea Guinea na kuwasili mji wa kibiashara wa Abijan, Corte D'Voire tarehe 12 Agosti 2021. 
Mgonjwa alilazwa hospitalini baada ya kupata homa na anaendelea na kupatiwa matibabu. 
"Inatia wasiwasi sana kwamba mlipuko huu umetangazwa huko Abidjan, jiji kuu la biashara lenye zaidi ya watu milioni 4," amesema Dk Matshidiso Moeti, na kuongeza kuwa. "Hatahivyo, tuna utaalamu mkubwa ulimwenguni kwas asa wa kukabiliana na Ebola uko hapa barani Afrika. I Corte D'Voire inaweza kutumia uzoefu huu na kuleta majibu kwa kasi kamili. Nchi hii ni moja kati ya sita ambazo WHO tumesaidia hivi karibuni kuimarisha utayari wao wa kukabiliana na Ebola, na utambuzi huu wa haraka wa mgonjwa unaonesha utayari unafaidika.”
Kwa mwaka huu mlipuko wa Ebola umetangazwa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo- DRC na  Guinea lakini ni mara ya kwanza mlipuko kutoka katika mji mkubwa kama Abijan tangu mlipuko lipotokea Ukanda wa Magharibi mwaka 2014-2016.

Wahudumu wa afya wakivaa vifaa vya kujikinga kabla ya katika kituo ambacho watu wanaoshukiwa kuwa na Ebola wamewekwa katika karantini kuweza kufanyiwa uchunguzi na uangalizi na kisha kupatiwa matibabu . Ni kituo cha muda cha ebola (Januari 2019)
World Bank/Vincent Tremeau
Wahudumu wa afya wakivaa vifaa vya kujikinga kabla ya katika kituo ambacho watu wanaoshukiwa kuwa na Ebola wamewekwa katika karantini kuweza kufanyiwa uchunguzi na uangalizi na kisha kupatiwa matibabu . Ni kituo cha muda cha ebola (Januari 2019)

 

  Kukabiliana na mlipuko zaidi 

Ebola ni ugonjwa hatari ambao mara vingi husababisha vifo vya binadamu na nyani. Viwango vya vifo vitokanavyo na Ebola ni kati ya 25% hadi 90% kwa milipuko iliyotokea zamani. Hivi sasa baada ya tafiti nyingi kuna matibabu madhubuti yanayopatikana na ikiwa wagonjwa wanagundulika na kupatiwa matibabu mapema, pamoja na huduma za uangalizi, uwezo wa kupona ugonjwa huo huongezeka maradufu.
 
WHO inasaidia kuratibu shughuli za kukabiliana na Ebola mpakani na tayari dozi za chanjo 5000 za Ebola ambazo shirika hilo lilisaidia kukabiliana na mlipuko nchini Guinea zinasafirishwa kupelekwa Corte D'Voire kufuatia makubaliano kati ya wizara za afya za Corte D'Voire na Guinea. 

Ndege Kutoka Abidjan inaenda kuchukua chanjo ambazo zitatumika kuchanja watu walio katika hatari kubwa, pamoja na wafanyikazi wa afya, watoa huduma ya kwanza Pamoja na watu waliokutana  na mgonjwa kwa mara ya kwanza .
Pamoja na kutangazwa mlipuko wa Ebola nchini Corte D'Voire kulingana na kanuni za kimataifa za afya, lakini WHO haishauri vizuizi vyovyote vya kusafiri kwenda na kutoka nchini humo.

WHO imesisitiza wakati nchi zinaendelea kupambana na janga la COVID-19, zinapaswa kuimarisha utayari wao kwa kukabiliana na visa vya Ebola.