Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yamuomboleza aliyekuwa mwandishi wa hotuba wa Kofi Annan 

Katibu Mkuu Kofi Annan (Kushoto) akijadiliana jambo na timu yake akiwemo Edward Mortimer (wa 2 kushoto) kuhusu hotuba ya Iraq Machi 2003
UN Photo/Stephenie Hollyman
Katibu Mkuu Kofi Annan (Kushoto) akijadiliana jambo na timu yake akiwemo Edward Mortimer (wa 2 kushoto) kuhusu hotuba ya Iraq Machi 2003

UN yamuomboleza aliyekuwa mwandishi wa hotuba wa Kofi Annan 

Masuala ya UM

“Ukiweka viwango utadumu kwa muda mrefu” ni moja ya kauli zilizowahi kutolewa na Edward Mortimer aliyekuwa mwandishi mkuu wa hotuba za Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan. 

Mortimer ameaga dunia mwishoni mwa wiki na sasa kwenye Umoja wa Mataifa , marafiki na wafanyakazi wenzake wa zamani wanamuomboleza. 

Wakati wake akifanya kazi hiyo kati ya mwaka 1998 na 2006, ulikuwa ni wakati wa kipindi muhimu sana kwenye Umoja wa Mataifa baada ya vita Baridi, viliyotawaliwa na Vita vya Iraq, na athari za bomu lililoanguka kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Baghdad, mnamo mwaka 2003. 

Mkunjo wa miguu, kijito cha maneno 

Edward Mortimer mwandishi wa hotuba, mshausri wa sera na mkurugenzi wa mawasiliano wa Katibu Mkuu wa zamani wa UN, Kofi Annan
Photo: Video screen capture
Edward Mortimer mwandishi wa hotuba, mshausri wa sera na mkurugenzi wa mawasiliano wa Katibu Mkuu wa zamani wa UN, Kofi Annan

"Nakumbuka wazi kuwasili kwa Edward alikuwa na kelele za miguu ya kijambazi, nywele za mviringo zisizodhibitiwa na, zaidi ya yote, alikuwa ni mto wa maneno", anakumbuka Richard Amdur, ambaye sasa ni mkurugenzi wa uandishi wa hotuba katika Umoja wa Mataifa.  

Ameongeza kuwa “Alikuwa miongoni mwa genge la watu wenye akili waliomzunguka Katibu Mkuu, aliyepewa leseni ya kufikiria na kujaribu kuandika wakati ambapo, bado ilikuwa ni katika miaka ya awali ya kipindi cha baada ya vita baridi, akitoa taswira ya wakati ujao wa Umoja wa Mataifa ambao ulikuwa ukiandikwa upya na bado ulikuwa umejaa matumaini.” 

“Alikuwa mchangamfu, mcheshi, mwenye kuvutia na mwaminifu. Aliukumbatia Umoja wa Mataifa, akacheka na vichwa vya viongozi kwenye televisheni kututetea, na alijitoa kimasomaso kwa Kofi. Sauti yake kunyamazishwa sasa ni hasara kubwa, lakini kauli na maneno yake yaliweka kiwango wakati huo na yatadumu kwa muda mrefu.” 

Kwenye mkutano wa kila siku wa Umoja wa Mataifa na waandishi mjini New York, siku ya Jumatatu Stéphane Dujarric, Msemaji wa Umoja wa Mataifa, alimwelezea Bwana Mortimer kama "Mshauri anayeaminika wa Katibu Mkuu na mlinzi hodari wa Umoja wa Mataifa ambaye alitengeneza alama ya mafanikio ya miradi na mipango ya Annan. ” 

Kama watu tuliyefanyanae kazi tulikuwa na bahatiya kufanyakazi bega kwa bega na mtu ambaye alikuwa Hodari na mwenye akili sana na mtumiaji mzuri wa maneno na kipawa fulani na ambaye daima alithamini wanafanyakazi wengine na kuwapenda.” 

Bahati na heshima kubwa 

Jaya Dayal, mkuu wa wafanyikazi katika Idara ya Mawasiliano ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa, alifanya kazi kwa karibu na Bwana Mortimer kama msaidizi wake maalum kati ya mwaka 2002 na 2006. Alielezea kipindi hicho kama "bahati", na kuongeza kuwa "Edward alituonyesha jinsi katikak kazi yetu, na pia katika maisha yetu ya kila siku, tunavyoweza kuheshimu utu wa kila mwanadamu katika ulimwengu usiokamilika wenye maumivu. Kazi yetu kwa pamoja ilipunguzwa na uchangamfu wake mkubwa na ukarimu aliotuonyesha kila mmoja wetu, na hiyo ilitufanya tujihisi kama watu maalum katika kazi yetu.” 

Mwanahabari wa zamani wa magazeti ya Times, na Financial Times, na mwandishi wa vitabu vinavyozingatia sana juu ya Uislamu na chama cha Kikomunisti cha Ufaransa, Bwana Mortimer, alijiunga na wafanyikazi wakuu wa Bwana Annan haswa kwa udadisi, kama alivyoelezea katika mahojiano na UN News aliyoyafanya mwaka 2014  

Edward Mortimer, mwandishi mkuu wa hotuba wa Katibu Mkuu wa zamani Kofi Anan akifuatilia hotuba iliyokuwa ikirekodiwa na Annan
UN Photo/Stephenie Hollyman
Edward Mortimer, mwandishi mkuu wa hotuba wa Katibu Mkuu wa zamani Kofi Anan akifuatilia hotuba iliyokuwa ikirekodiwa na Annan

Mtazamo mpya 

"Nilitaka kuona jinsi ulimwengu ulivyo kutoka mahali hapa pazuri. Kwa kweli nilifurahi sana kupewa kazi hiyo, lakini nilihisi kwamba wangenichukua nilivyo Nilisema kile nilichofikiria, haswa katika mikutano ya ndani. Na nadhani kwamba, kwa ujumla, hiyo ilithaminiwa kuwa muhimu. " 

Kutoka kwenye maisha yaliyozingatia elimu , na kujikita katika uandishi wa habari wa magazeti, wengine walitilia shaka ikiwa Bwana Mortimer atakuwa mtu sahihi kuwa mwandishi wa sauti ya mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa , lakini alibadilika haraka 

 “Nilipaswa kurahisisha mtindo wangu na kuandika masuala, sentensi ndefu na vifungu vya chini haviendi sanjari na vizuri katika hotuba. Nadhani mojawapo ya fhulka za Kofi Annan, ni kwamba anapenda kuelezea mambo kwa njia rahisi. Kwa hivyo, ilikuwa muhimu kuandika sentensi fupi na sio maneno mengi sana.” 

Dunia inahitaji kupata mtu bora wa kufanya kazi hiyo 

 Katika mahojiano yake na UN News mwaka 2014 Bwana Mortimer alikuwa akikosoa mchakato ambao Katibu Mkuu huchaguliwa, na akataka njia ya uwazi na iliyojumuishi ianzishwe. 

"Nadhani kuna kitu kwa kila mtu kufanya hapa kubadilisha mchakato huu na kuhakikisha kwamba tunamtafuta mtu bora wa jinsia yoyote, utaifa wowote ambaye atafanya kazi bora kwa ajili ya dunia. Hii ni kazi ya kipekee na ni jukumu kubwa sana. Na ulimwengu unahitaji kupata mtu bora wa kufanya kazi hiyo.” 

"Nadhani kuna mengi ya kusemwa, badala ya kuwa na kipindi cha miaka mitano kinachoweza kurejeshwa, muhula wa miaka saba usioweza kurejeshwa ungefaa ili Katibu Mkuu aendelee na kazi hiyo bila tuhuma ya kuwa anafanya upendeleo na ana mamlaka makubwa ili kujaribu kuhakikisha anachaguliwa tena. ” 

Baada ya kutoka Umoja wa Mataifa , Bwana Mortimer alijiunga na shirika lisilo la kiserikali la Salzburg global seminar, lililoko katika mji wa Austria, kama makamu wa rais mwandamizi na afisa mkuu wa programu.  

Alikuwa pia mwandishi mkuu wa ripoti ya Baraza la Ulaya juu ya ujumuishaji wa jamii za wahamiaji wanaoingia Ulaya na Amerika ya Kaskazini. 

Ameacha mkewe, Elizabeth, watoto wanne, na wajukuu saba.