Amani ni rasilimali adimu ambayo wengi wanaililia:Muhudumu wa kujitolea Gbambi

Sera ya Umoja wa Mataifa ya kutovumilia kabisa ukatili na unyanyasaji wa kingono
United Nations
Sera ya Umoja wa Mataifa ya kutovumilia kabisa ukatili na unyanyasaji wa kingono

Amani ni rasilimali adimu ambayo wengi wanaililia:Muhudumu wa kujitolea Gbambi

Masuala ya UM

Kutana na mfanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Jason William Gbambi ambaye anafanyakazi kama afisa uhamasishaji wa timu ya maadili na nidhamu ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS. Anasema kufanyakazi ya kujitolea ni kukumbatia jamii na kutambua mahitaji yao na hasa amani ambayo ni adumu nchini humo. Flora Nducha na taarifa zaidi 

 Nchini Sudan Kusini Jason Gbambia mfanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa  anayefanyakazi ya katika timu ya maadili na nidhamu ikijikita na ukatili na unyanyasaji wa kimngono anafafanua zaidi wanachokifanya “Hasa hasa jukumu letu kubwa ni kwenda nje kwenye jamii kuwapa mafunzo makundi mbalimbali kama wanawake, vijana, viongozi wa kijamii na pia maafisa wa serikali kuhusu hatari za unyanyasaji wa kingono katika jamii.” 

wasichana nchini Sudan Kusini wakihamasishwa kusoma na mmoja wa wafanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa UNMISS nchini humo
UNMISS/Denis Louro
wasichana nchini Sudan Kusini wakihamasishwa kusoma na mmoja wa wafanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa UNMISS nchini humo

Gbambi anasema kazi yake ina mitihani mingi lakini kubwa zaidi ni“Mvutano baina ya sera za Umoja wa Mataifa na mila na desturi za jamii na utamaduni wao, na hasa changamoto za COVID-19 zimekuwa tatizo kwetu sote, hasa wakati wa kufungwa kila kitu na watu kusalia majumbani ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo, wakati huo hatukuweza kwenda  kwenye maeneo mengine ya vijijini ambayo tunapaswa kwenda na kutoa mafunzo kwa baadhi ya washirika wetu.” 

Na mbali ya hilo“Amani ni rasilimali ambayo wakati mwingine ni adimu sana, kila mtu anahitaji amani na wakati tunapoishi kwenye mazingira ambayo amani haipo, maana yake ni lazima kuwe na mtu ambaye ataleta amani, na vijana wana uwezekano huo, kufikiria kusoma kwa sababu kupitia elimu wanaweza kujijengea ujuzi utakaowasaidia kuelewa thamani ya amani.” 

Gbabmbi ambaye ni mlemavu anayetembea na gogo anasema ulemavu wake haukumzuia kutimiza ndoto ya kwenda shule na kujitolea katika nchi yake kuwasaidia wengine na kwake hakuna jukwaa zuri kama kuwa mfanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa ambalo limempa fursa ya kuzifikia jamii nyingi ambazo hakuwahi hata kufikiria na zaidi ya yote ameelewa zadi utamaduni wake kama raia wa Sudan Kusini na sera za Umoja wa Mataifa hali ambayo inamuongezea weledi katika kazi yake.