Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Uchunguzi wa ebola.

Ebola yatangazwa kuisha rasmi nchini Guinea, WHO yawapongeza

Photo OMS/T. Jasarevic
Uchunguzi wa ebola.

Ebola yatangazwa kuisha rasmi nchini Guinea, WHO yawapongeza

Afya

Ugonjwa wa Ebola umetangazwa kumalizika rasmi hii leo nchini Guinea. 

Taarifa iliyotolewa na shirika la Afya ulimwenguni WHO kutoka Brazzaville Conakry imesema ugonjwa huo uliokuwa umemalizika mwaka 2016 uliibuka upya February 14 mwaka huu 2021 baada ya watu watatu kugundulika huko katika kijiji cha  Gouecke kilichoko Kusini mwa mkoa wa N’zerekore. 

Mkoa wa N’zerekore ndio ulikuwa wakwanza kugundulika mgonjwa wa Ebola kabla haujasambaa katika nchi jirani za Liberia, Sierra Leone na nyingine katika ukanda wa Afrika Magharibi kati ya mwaka 2014 mpaka 2016.
Jumla ya visa 16 vilithibitishwa na visa 7 viliripotiwa katika mlipuko wa hivi karibuni nchini Guinea ambapo wagonjwa 12 walipoteza maisha na wengine 11 walinusurika na ugonjwa huo unaotajwa kuwa moja kati ya magonjwa hatari duniani. 
Muda mfupi baada ya kutangazwa kwa ugonjwa huo idara ya afya ya nchi hiyo kwa kushirikiana na WHO pamoja na wadau wengine waliandaa mpango wa Haraka wa kukabiliana na ugonjwa huo kwa kutumia uzoefu walioupata wakati wanakabiliana na tatizo hilo nchini humo pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC. 
Nikutokana na juhudi hizi hii chini ya miezi sita wameweza kumaliza tatizo  na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus amesifu juhudi hizo .” Ninawapongeza wanajamii walio athirika, serikali ya Guinea , Wafanyakazi wa sekta ya Afya, mashirika mengine yaliyoshiriki kusaidia pamoja na kila mtu ambaye juhudi zake za kukabiliana na ugonjwa huu zimewezesha kukabiliana nao.” 
Ameongeza kuwa “WHO itaendelea kuwasaidia wagonjwa waliopona kupata huduma baada ya ugonjwa lakini serikali ya nchi hiyo ipo tayari kupambana na ugonjwa huo iwapo utaibuka tena. “ Kulingana na mafunzo tuliyoyapata kutoka kwenye mlipuko wa mwaka 2014 mpaka 2016 na kwa juhudi za haraka zilizo ratibiwa ambazo zilishirikisha jamii, mipango kabambe ya sekta ya afya kwa umma, na utumiaji sahihi wa chanjo, nchi ya Guinea imeweza kudhibiti mlipuko huo kuenea nchini kwake na nje ya mipaka yake.”

Chanjo ya Ebola yaanza nchini Guinea ili kuzuia mlipuko mpya.
WHO
Chanjo ya Ebola yaanza nchini Guinea ili kuzuia mlipuko mpya.


  Msaada uliotolewa na WHO

Shirika hilo la Afya ulimwenguni lilisafirisha chanjo za Ebola 24,000 kwenda nchini humo na kisha kusaidia kuwapa chanjo takriban watu 11,000 ambao walikuwa kwenye hatari ya kupata maambukizi ikiwemo wafanyakazi wa idara ya afya 2800 waliokuwa mstari wa mbele kutoa huduma. 
Zaidi ya wataalamu 100 wa WHO pia walikuwa nchini humo wakitoa msaada ya namna ya kuhakikisha wanaukabili ugonjwa huo na kuzuia usieneee maeneo mengine ambapo walitoa chanjo, kutibu wagonjwa kwakutumia aina mpya ya dawa na kuendelea kuwafuatilia. Mshikamano na jamii ulisaidia sana kuwapatia elimu kuhusu kirusi cha ebola hivyo ushiriki wao moja kwa moja wa kupambana ulisaidia kumaliza ugonjwa huo. 
“Ingawa hiii Ebola imeibuka tena katika eneo lile lile la Afrika Magharibi ambapo liliuwa watu 11,000 tunashukuru mbinu mpya za kibunifu na mafunzo tuliyopata awali wakati wa kukabiliana nao, Guinea imeweza kudhibiti kirusi hiki ndani ya miezi 4” amesema Dkt Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO katika bara la Afrika. 
Ameongeza kuwa “tunazidi kukabiliana kwa haraka, kwa ubora na ufanisi katika kupambana na Ebola. Lakini wakati mlipuko huu umemalizika, ni lazima kuendelee kuchukua tahadhari juu ya uwezekano wa kutokea tena na kuhakikisha utaalamu wetu katika kukabiliana na Ebola unapanuka na kusaidia kupambana na magonjwa mengine ya kiafya kama vile coronavirus">COVID-19” 
Ingawa Guinea pekee ndio iligundulika kuwa na wagonjwa, WHO katika kuhakikisha wagonjwa hawavuki mpaka na kwenda kuambukiza nchi nyingine walifanya kazi na mataifa jirani 6 kujiandaa kukabiliana na ugonjwa huo iwapo utaibuka ikiwemo kufanya uchunguzi wa kiafya kwa watu wanaovuka mipaka katika jamii zilikuwa hatariki zaidi kuambukizwa pamoja na kuleta ushirikiano baina ya nchi hizo na huduma za afya. 

Mlipuko wa ebola umeripotiwa nchini Guinea. (Maktaba)
WHO/Junior D. Kannah
Mlipuko wa ebola umeripotiwa nchini Guinea. (Maktaba)


  Kuwafuatilia waliopona Ebola 

Usaidizi kwa waliopona Ebola ni jambo muhimu. Uchunguzi umeonesha kirusi kilichoikumba Guinea mwaka huu kinafanana na kile cha mwaka 2014 mpaka 2016 wakati ugonjwa huo ulipoibuka kwa mara ya kwanza. Ingawa bado stadi nyingi zinatakiwa kufanyika kuhusu ugonjwa huu, tayari serikali ya Guinea imeanzisha programu maalum ya kuwafuatilia manusura wa Ebola ili kuwapatia msaada wa muda mrefu. 
Katika kuisaidia serikali katika mkakati wake huo WHO inashirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa pamoja na mengine mengi kuhakikisha jamii inapata msaada wa haraka na kurejea maisha yao ya awali.