Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baba alimkimbia mama kwa madai kwamba hawezi zaa mtoto kama mimi-Mwaura

Mwasisi wa halmashauri ya watu wenye ualbino Kenya. Mbunge na Seneta wa kwanza wenye ualbino nchini Kenya.
UN News/Grece Kaneiya
Mwasisi wa halmashauri ya watu wenye ualbino Kenya. Mbunge na Seneta wa kwanza wenye ualbino nchini Kenya.

Baba alimkimbia mama kwa madai kwamba hawezi zaa mtoto kama mimi-Mwaura

Haki za binadamu

Mazingira ambayo nimekulia mimi yalikuwa ya sintofahamu kwa sababu ya suala nzima kwamba nimezaliwa tofauti katika familia yangu, watu wa familia yangu walikuwa na tetesi kuelewa kwa nini nilizaliwa nilivyo na babangu alimkimbia mama kwa madai kwamba hawezi zaa mtoto kama mimi.

 

Soundcloud

Hiyo ni kauli ya Isaac Mwaura, mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualbino ambaye pia ni mbunge wa kwanza na seneta nchini Kenya mwenye ualbino.
Bwana Mwaura anasema unyanyapaa alianza pale babake alipoondoka kw sababu yake, pia ailiazimika kwenda shule ya malezi akiwa na umri mdogo, “ilikuwa ni lazima twende shule kwa sababu shule pekee ya watu wasioona ya Thika ndio ilikuwepo katika wilaya yangu ya Kiambu lakini kule kutengana na mama yangu wakati huo kulikuna na chungu hatahivyo kulikuwa kujumuika vizuri na wanafunzi kutoka kona zote za nchi na suala la utaifa likawa limebobea sana na tukawa na utengamano mzuri”
Miaka ya themanini uelewa kuhusu watu wenye ualbino ulikuwa hafifu huku suala la kupaka mafuta ya kujikinga dhidi ya jua likionekana kama kitu cha fahari kwa ajili ya kujistarehesha kwa watalii kwani elimu kuhusu bidhaa hizo haikuwepo aidha bei yake ilikuwa ngumu kumudu. Isitoshe bwana Mwaura anasema jamii ilikuwa na unyanyapaa, “wakati ukitembea mtaani unakuta watu wanasema mambo ya kuudhi kukuhusu.”
Licha ya hayo bwana Isaaca anasema, “tajriba ya uongozi kwangu ilijitokeza nikiwa mtoto mdogo wakati niko chekechea.” Alishikilia nyadhfa mabli mbali hadi akiwa chuo kikuu cha Kenyatta ambapo anasema, “nikachaguliwa kama kiongozi wa wanafunzi katika mwaka wa kwanza wa kujiunga nikawa mtu wa kwanza wenye ualbino kuwahi shika nafasi hiyo na uanavuguvugu wangu ukaendelea na nikachangia katika baraza la kitaifa la watu wenye ulemavu na na ndiposa nikaweza kutoa uelewa kwa watu kwamba ualbino ni ulemavu kwani awali ulikuwa unajumuishwa kwenye watu wasioona lakini tunabaguliwa kutokana na rangi ya ngozi yetu.”
Bwana Mwaura anasema ndoto ya kuwa mbunge ilichangiwa na kwamba wakati angali mdogo mama na bibi yake walikuwa wakifanya kazi katika shamba la mbunge wa eneo hilo kwa hiyo sifa na umaarufu wake ulimvutia hatahivyo sio kila mtu aliamini kwamba angetimiza ndoto hiyo.
Licha ya hatua ambazo zimekwisha patikana lakini, bwana Mwaura anasema bado safari ni ndefu akisema, “kama nyumba msingi upo lakini bado hatujafika ndipo.”