Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wito wangu kwa jamii ni tupendane tu bila kujali hali zetu-Mwigulu 

Jimboni Equateur nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ulemavu wa ngozi ni jambo la kawaida na jamii hujumuika pamoja.
UN /Marie Frechon
Jimboni Equateur nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ulemavu wa ngozi ni jambo la kawaida na jamii hujumuika pamoja.

Wito wangu kwa jamii ni tupendane tu bila kujali hali zetu-Mwigulu 

Haki za binadamu

Licha ya kupungua kwa vitendo vya mashambulizi dhidi ya watu wenye ualbino, bado kundi hilo linaishi kwa mashaka na hofu kutokana na madhila wanayopitia katika maisha yao ya kila siku.

Miongoni mwao ni mtoto mtanzania Mwigulu Matonange Magesa ambaye sasa ana umri wa miaka 16, na ambaye mashambulizi dhidi yake yamemsababishia kupoteza mkono wake mmoja katika kisa hiki anachosimulia alipohojiwa na Priscilla Lecomte wakati alipotembelea New York, MArekani hivi karibuni kushiriki mkutano wa kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya watu wenye Ulemavu.

Kijana Magesa amesimulia namna ambavyo watekelezaji wa uhalifu ambao ulimuacha yey bila mkono ulivyopangwa huku wahalifu hao wakidai kwamba wanahitaji msaada wake kumsaidia kusaka mifugo wao. Licha ya hatari iliyomkabili lakini kijana Magesa alinusurika kifo na hata kuhamishwa kutoka kijijini hadi Dar es Salaam ambako anasema kwa bahati nzuri wanafunzi na watu kwa ujumla wana uelewa zaidi kuhusu ualbino na hivyo hali sio kama ya awali. 

Kijana Magesa amesema ana ndoto kubwa pia katika siku za usoni basi kwa undani zaidi sikiliza makala yote.