Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunapoichafua bahari tunaumia wenyewe: Guterres

Samaki wakiwa kwenye eneo lenye matumbawe  kwenye bahari ya Pasifiki
Ocean Image Bank/Jayne Jenkins
Samaki wakiwa kwenye eneo lenye matumbawe kwenye bahari ya Pasifiki

Tunapoichafua bahari tunaumia wenyewe: Guterres

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Leo ni siku ya ya Bahari duniani, katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa maadhimisho ya siku hii, ametoa wito wa kuacha kuchafua bahari kwani inaathiri zaidi wanufaika wake ambao wengi ni wafanyabiashara wadogo kutoka nchi zinazo endelea.

Tweet URL

Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho ya siku ya Bahari duniani ni “Bahari: Maisha na Kipato”, lengo likiwa ni kusisitiza umuhimu wa kulinda baharí kwani inasaidia kwenye maisha ya kitamaduni na kiuchumi ulimwenguni kote.

katika ujumbe wake kwa njia ya video Guterres amehimiza kukomeshwa kwa uchafuzi wa baharí “Tathmini ya pili iliyofanyika hivi karibuni ya Bahari Ulimwenguni ilithibitisha kuwa pamoja na faida nyingi ambazo bahari hutoa kwa wanadamu lakini ni sisi ndio tunaidhoofisha kwa matendo yetu wenyewe." 

Pia ameeleza masikitiko yake jinsi baharí zinavyosongwa na taka za plastiki, ambazo zinaonekana kila kona iwe kwenye matumbawe hadi kina cha bahari. Zaidi ya watu bilioni tatu wanategemea bahari kupata mapato yao, idadi kubwa wakiwa katika nchi zinazoendelea.

Akizungumzia suala la upotevu wa fecha amesema “ Uvuvi kupita kiasi unasababisha upotevu wa karibu dola bilioni 90 kila mwaka katika faida- ambayo pia huongeza hatari kwa wanawake, ambao ni muhimu kwa ustahimilivu wa biashara ndogo ndogo za uvuvi.” 

Katibu mkuu huyu wa UN amegusia umuhimu wa kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, kukaribia kufikia lengo la kiwango cha digrii 1.5 cha Mkataba wa Paris, na kuhakikisha afya ya bahari kwa sasa na vizazi vijavyo. 

Maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Bahari Duniani yanakuja wakati ulimwengu unakabiliwa na ugonjwa wa COVID-19, janga la hali ya hewa na kuendelea kwa uharibifu wa rasilimali za bahari na majini utokanao na binadamu.