Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu na sayari dunia ‘vitagongana’ isipochukuliwa hatua-UNDP 

Mtoto akibeba kapu la matunda katika mtaa wa Cotonou uliofurika kwenye mji wa bandari wa Benin.
UNICEF/Oliver Asselin
Mtoto akibeba kapu la matunda katika mtaa wa Cotonou uliofurika kwenye mji wa bandari wa Benin.

Watu na sayari dunia ‘vitagongana’ isipochukuliwa hatua-UNDP 

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP kupitia ripoti yake mpya limeonya kuwa nchi lazima zibuni njia zao za maendeleo ili kupunguza uharibifu wa mazingira na ulimwengu wa asili, la sivyo ni kuhatarisha maendeleo ya ubinadamu kwa ujumla. 

Janga la virusi vya corona ni tatizo la hivi karibuni linaloukabili ulimwengu, na jamii kila mahali zinahitaji "kuachilia nguvu zao juu ya asili", au la kuingia katika hatari zaidi kama hiyo ya janga la corona, UNDP imeeleza katika ripoti ya mwaka huu ya Maendeleo ya Binadamu iliyotolewa hii leo Jumanne ikiitwa, The Next Frontier yaani Mpaka au kizingiti kinachofuata.  

Mkuu wa UNDP Achim Steiner amesema, “wanadamu wana nguvu zaidi juu ya sayari (Dunia) kuliko wakati mwingine wowote. Baada ya coronavirus">COVID-19, joto linalovunja rekodi na kukosekana kwa usawa, ni wakati wa kutumia nguvu hiyo kufafanua kile tunachomaanisha kwa maendeleo, ambapo nyayo zetu za ukaa na matumizi si kificho tena."  

Aidha Bwana Steiner amesema kama ripoti hii inavyoonesha, hakuna nchi yoyote duniani ambayo imefikia  maendeleo ya juu sana ya binadamu bila kuweka shida kubwa kwenye dunia. Lakini tunaweza kuwa kizazi cha kwanza kurekebisha kosa hili. Hiyo ndiyo mipaka inayofuata ya maendeleo ya binadamu. 

Kushirikiana na asili 

UNDP inasema mafanikio katika maendeleo ya binadamu, "yatahitaji kufanya shirikiana na sio yawe dhidi ya asili, wakati yanabadilisha au kuboresha kanuni za kijamii, maadili, na serikali na motisha za kifedha." 

Kwa mfano, makadirio yanaonyesha kwamba kufikia mwaka 2100, nchi maskini zaidi ulimwenguni zinaweza kupata hadi siku 100 zaidi za hali ya hewa mbaya kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi kila mwaka  idadi ambayo inaweza kukatwa nusu ikiwa Mkataba wa Paris juu ya mabadiliko ya tabianchi utatekelezwa kikamilifu. 

Vivyo hivyo, upandaji miti na utunzaji bora wa misitu peke yake inaweza kuwa karibu robo ya vitendo vya kabla ya mwaka 2030 vinahitajika kuzuia kuongezeka kwa joto duniani kufikia nyuzi joto 2 za selisiasi juu ya viwango vya joto vya  kabla ya viwanda, ripoti inabainisha. 

Jua likichomiza kutoka umbali wa mita 5000 nyuma ya mlima Iztaccihualt nchini Mexico
Picha na WMO/Miguel Angel Trejo Rangel
Jua likichomiza kutoka umbali wa mita 5000 nyuma ya mlima Iztaccihualt nchini Mexico

Kuondoa ukosefu wa usawa 

Ripoti hiyo pia inaelezea athari za kukosekana kwa usawa kati ya nchi na ndani ya nchi, ukosefu wa ushiriki wa watu wa asili katika kufanya uamuzi, na ubaguzi, ikiacha jamii zilizoathiriwa zikiwa katika hatari kubwa za mazingira. 

Ripoti imeongeza kuwa kupunguza mashinikizo ya dunia kwa njia inayowezesha watu wote kufanikiwa katika enzi hii mpya inahitaji kuondoa kukosekana kwa usawa mkubwa wa nguvu na fursa ambayo inasimama katika mabadiliko.