Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Baraza la usalama likikutana na shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lakaribisha makubaliano ya viongozi wa Somalia 

UN Photo/Loey Felipe
Baraza la usalama likikutana na shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lakaribisha makubaliano ya viongozi wa Somalia 

Amani na Usalama

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamepongeza uamuzi uliofikiwa Mei 27 2021, na viongozi wa nchi ya Somalia baada ya Waziri mkuu wa nchi hiyo Mohamed Hussein Roble kuitisha mkutano wa kutekeleza makubaliano waliyojiwekea September 17 juu ya kuwa na uchaguzi mkuu wa kihistoria. 

Wajumbe wa Baraza mewapongeza viongozi wa nchi ya Somalia kwa kuweka utulivu, usalama na maendeleo, na kuweka maslahi ya wananchi wa nchi hiyo mbele. 
 
Pia wamekaribisha ahadi ya kuwa na uchaguzi wa amani, jumuishi na wakuaminiwa, ambao unaheshimu makubaliano ya kuwa na kiwango cha wanawake bungeni, wasiopungua asilimia 30. 
 
Wajumbe hao pia wamewahimiza viongozi wa Somalia, kuhakikisha wanaendeleza muelekeo huu mzuri wa sasa, ili uchaguzi uweze kufanyika ndani ya kipindi cha siku 60 kama walivyo kubaliana. 
 
Wamehimiza pande zote kuendelea kushirikiana kwa uwazi na  kwaminajili ya kujenga,  ili kama changamoto yeyote itajitokeza iweze kutatuliwa kwa haraka. Pia wamekaribisha  makubaliano ya kuanzishwa kwa utaratibu maalum wa kusuluhisha mizozo kwa amani. 
 
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamepongeza msaada uliotolewa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM, na Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM, na kuwapongeza kwa jinsi nchi inavyojiandaa kwa ajili ya uchaguzi, kutekeleza malengo yaliyoanishwa kwenye kiambatanisho cha mazungumzo ya tarehe 27 Mei, na wanaendelea kuwasiliana kuhakikisha wanaleta mabadiliko kwa usalama nchini Somalia, kama yanavyoitwa UNSCR 2568(2021).
 
Wajumbe wa Baraza la Usalama wamethibitisha heshima yao kwa uhuru wa nchi, uhuru wa kisiasa kuheshimu mipaka  na umoja wa Somalia