Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo kati ya Hargesa na Moghadishu ni dalili njema: Swan

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, James Swan akihutubia Baraza la Usalama.
UN Photo/Manuel Elías
Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, James Swan akihutubia Baraza la Usalama.

Mazungumzo kati ya Hargesa na Moghadishu ni dalili njema: Swan

Amani na Usalama

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia na mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSOM leo amezuru Hargesa Somaliland na kukutana na viongozi wa eneo hilo kujadili uchaguzi na maendeleo.

Bwana. James Swan ambaye amezuru eneo hilo baada ya kuwa huko mara ya mwisho miezi sita iliyopita amekutana na Rais Musa Bihi Abdi na timu yake wakiwemo mawaziri, wawakilishi wa asasi za kiraia , viongozi wa vyama vya siasa na washirika wa kimataifa wanaofanyakazi Somaliland.

Katika majadiliano yao Swan ameishukuru serikali ya Somaliland kwa miradi ambayo amesema inalenga kujenga kujiamini na kuchagiza majadiliano baina ya utawala Hargesa na serikali kuu Moghadishu. "Tunaamini kuna maeneo mengi ambayo ushirikiano mkubwa unaweza kusaidia kuimarisha usalama, kuchagiza ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya watu.”

Mwakilishi huyo ambaye pia alizuru miradi mbalimbali ikiwemo wa ujuzi kwa ajili ya watu wenye ulemavu na wa uokozi wa wanyamapori amesema Tumetiwa moyo na hatua zilizopigwa katika mchakato wa kukamilisha hatua zote muhimu kwa Somaliland kufanya uchaguzi wa Bunge 2020. Tunakaribisha majadiliano miongoni mwa chama na kutoa wito wa utekelrezaji wa makubaliano ya karibuni ambayo yatawezesha maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu wa 2020Tunatoa wito kwa uongozi wa Somaliland kuhakikisha uhuru wa kuongea na kukusanyika unaheshimiwa , pamoja na uqwezo wa vyama vya siasa kujiandaa na kufanyakazi. Uwanja huo wa kisiasa ni muhimu kwa kuwa na mchakato unaoaminika.”

Swan ameongeza kuwa pia wameona juhudi chanya za karibuni kushughulikia changamoto za muda mrefu katika maeoneo ya Sool na Sanaag ikiwemo baada ya mapigano ya Tukarag mwaka 2018 kwa kupitia majadiliano na mtazamo nbora ili kupunguza hatari ya mgogoro zaidi.  Amesisitiza kwamba “Tunataka juhudi hizi kuendelea na kuimarishwa zaidi”

Amemuahidi Rais na watu wa Somaliland kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana nao kupitia miradi na program mbalimbali za Umoja wa Mataifa na mashirika yake ambapo kwa sasa yako 16 yakifanyakazi na kutoa msaada unaohitajika.