Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, Bwana James Swan, ametembelea jimbo la Galmudug.

Viongozi wa Somalia wahimizwa kuandaa uchaguzi mkuu

UN Photo/Omar Abdisalan
Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, Bwana James Swan, ametembelea jimbo la Galmudug.

Viongozi wa Somalia wahimizwa kuandaa uchaguzi mkuu

Amani na Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mkutano wa wazi kuhusu hali nchini Somalia.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric iliyotolewa mjini New York Marekani inasema, mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, James Swan, ameeleza kuwa shughuli za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu zimekumbwa na changamoto kadhaa katika miezi ya hivi karibuni.

Dujarric amewaeleza waandishi wa habari kuwa "Swan ametoa wito kwa viongozi wa Somalia kutafuta suluhu kwa nia njema na kuonesha aina ya uongozi nchi hiyo inayo uhitaji katika wakati huu wa kihistoria na kusisitiza makubaliano yaliyotiliwa saini Septemba 17 nilazima yafuatwe na viongozi wajikite kwenye kuandaa uchaguzi wa uwazi."

  
Swan amenukuliwa akisema hali ya usalama nchini Somalia inaendelea kuwa ya wasiwasi mkubwa, huku akisisitiza wanamgambo wa Al-Shabaab wanasalia kuhatarisha amani kwa kiasi kikubwa, na wenye uwezo wa kupanga na kutekeleza mashambulizi wakiilenga Somalia

Hali ya kibinadamu ni mbaya nchini humo ambapo, wasomali Milioni 5.9 ambao ni sawa na theluthi moja ya watu wote wa taifa hilo wana uhitaji wa misaada ya kibinadamu mwaka huu.