Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nia ya kupambana na Alshabab tunayo vifaa ndio mtihani: Uganda

Askari wa Uganda  wapewa medali nchini Somalia baada ya kumaliza mwaka wakiwa kazini chini ya kikosi cha AMISOM.
AMISOM/Omar Abdisalan
Askari wa Uganda wapewa medali nchini Somalia baada ya kumaliza mwaka wakiwa kazini chini ya kikosi cha AMISOM.

Nia ya kupambana na Alshabab tunayo vifaa ndio mtihani: Uganda

Amani na Usalama

Moja ya changamoto kubwa zinazokabili operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa ni vifaa ili kuwawezesha walinda amani kutimiza majukumu yao kwa ufanisi.

Kilio hicho kimewasilishwa na asilimia kubwa ya nchi wanachama zinazochangia vikosi wakati wa mjadala maalumu kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu operesheni za ulinzi wa amani na changamoto zake.

Uganda ni miongoni mwa mataifa yanayochangia vikosi ikiwemo katika operesheni za ulinzi wa amani za kikosi cha Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM.

Kikosi hicho kinasimamiwa kwa ushirikiano wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa . Kwa mujibu wa waziri wa mashauri ya kigeni wa Uganda, Okello Oryem, anayehudhuria mjadala huo hapa New York Marekani ,walinda amani wa Uganda wanachangamoto lukuki.aziri Okello Oryem

(SAUTI YA OKELLO OYREM)

Kwa mantiki hiyo amewasilisha ombi maalumu

(SAUTI YA OKELLO ORYEM)