Changamoto Somalia ni kuwa na taasisi zitakazokidhi wote:Keating

24 Januari 2018

Kundi la kigaidi la Al Shabbab linaendelea kuwa tishio nchini Somalia wakati serikali ikijaribu kujenga upya taasisi za usalama na kuifanya nchi hiyo kuweza kujitegemea. Hayo yamesemwa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating, alipozungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, ingawa pia amesema jitihada mbalimbali za kujenga serikali inayowajibika, na itakayowezesha watu wote zinaendelea.

Kundi la kigaidi la Al Shabbab linaendelea kuwa tishio nchini Somalia wakati serikali ikijaribu kujenga upya taasisi za usalama na kuifanya nchi hiyo kuweza kujitegemea. Hayo yamesemwa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating, alipozungumza na UN News, ingawa pia amesema "jitihada mbalimbali za kujenga serikali inayowajibika, na itakayowezesha watu wote zinaendelea.

Ameongeza kuwa wakati mpango wa Muungano wa Afrika wa kulinda amani nchini humo AMISOM umekuwa ukilinda mazingira ya kisiasa , lakini muafaka wa kisiasa ni lazima ufikiwe na fedha za ufadhili zipatikane kabla ya kuhamishia jukumu la usalama kwa jeshi la Somalia na kwamba

(MICHAEL KEATING CUT 1)

Changamoto hasa ni kujenga taasisi ambazo zitaaminiwa na Wasomali wote iwe ni polisi au jeshi, au elimu, kilimo, au mutawala wa sheria . tuko katikati ya juhudi mbalimbali za kujenga taifa la uwajibikaji litakalokidhi mahitaji ya wote.”

Na kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwaka 2020 Bwana Keating amesema

(MICHAEL KEATING CUT 2)

Umoja wa Mataifa unashirikiana na tume huru ya taifa ya uchaguzi na serikali kuwasaidia Wasomali kuandaa mpango wa kushughulikia changamoto mbalimbali ukihusisha wanasiasa, watu wanaosaidia kujenga uwezo wa taasisi ilizitekeleze majukumu yake hivyo Umoja wa Mataifa unahusika sanakwa kutumia ufadhili wa nchi wahisani kusaidia Wasomali kusonga mbele.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter