Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa UNDP wabadili maisha ya wanawake rasi ya Yucatan Mexico

Bidhaa mbalimbali za utunzaji wa kibinafsi, ikiwa ni pamoja na sabuni na chupa za shampoo na losheni, zinaonyeshwa kwenye meza ya mbao.
UNDP Mexico, SGP Mexico, Claudia Novelo Alpuch Asali ya Melipona na bidhaa zake nyingi, kama vile propolis, zinajulikana kwa kutumika katika tiba.

Mradi wa UNDP wabadili maisha ya wanawake rasi ya Yucatan Mexico

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kikundi cha wanawake wa Mayan kilichopo katika rasi ya Yucatan nchini Mexico kimeweza kujikwamua kiuchumi baada ya kupata mkopo kutoka Shirika la umoja wa Mataifa la Mpango wa maendeleo UNDP.

Kikundi hicho kinajishughulisha na ufugaji nyuki pamoja na uzalishaji bidhaa zitokanazo na mazao ya nyuki.

Mwanamke wa Mayan mwenye tabasamu ameshika chupa ya asali karibu na mzinga wa nyuki wa mbao.
UNDP Mexico, SGP Mexico, Claudia Novelo Alpuche María Keb Xool akionesha chupa ya asali ya melipona ambayo anauza.

 

Kupitia mafunzo mbalimbali waliyoyapata kupitia mitandao ya wadau wanakikundi wamejengewa uwezo wa kuzalisha asali bora na ukaguzi wa mara kwa mara wa kizinga ya nyuki.

Wanakikundi wote wanauwezo wa kukagua asali iwapo imefikia viwango vinavyotakiwa katika uzalishaji wa mazao yatokanayo na asali ambayo pia wanahusika moja kwa moja na utengenezaji wake.

Mazao wanayozalisha kutokana na bidhaa na mazao ya nyuki ni pamoja na sabuni, krimu za kupaka usoni, sabuni za kuosha nywele pamoja na Mafuta ya kujipaka.

 

Mwanamke wa Mayan ameshika kikapu cha wicker kilichojaa bidhaa asilia, ikiwa ni pamoja na asali na vipodozi.
UNDP Mexico, SGP Mexico, Claudia Novelo Alpuche Asali ya Melipona na bidhaa zake nyingi, kama vile propolis, zinajulikana kwa kutumika katika tiba.

Kwa mara ya kwanza wanawake hawa walikuwa hawajishughulishi na kitu chochote cha kuwaingizia kipato lakini kwa sasa kupitia kikundi chao wanaweza kuuza bidhaa na kujipatia kipato kwa ajili ya kujikimu na kusaidia familia.

Mkono unanyoosha mkono kwenye mzinga wa mbao ili kukagua sega la nyuki wasiouma, wanaojulikana kama asali ya melipona.
UNDP Mexico, SGP Mexico, Claudia Novelo Alpuche Wanawake wa Mayan wanaofuga nyuki kwenye Peninsula ya Yucatan

 

Biashara ya nyuki na mazao yake imewapa furaha wanawake hawa.

Mwanamke wa Mayan aliyevaa barakoa na blauzi ya maua anashikilia vitu vya mbao kwenye rafu zilizo chini ya paa la nyasi.
Claudia Novelo Alpuche/UNDP Mexico, SGP Mexico. Mwanachama wa mtandao wa wafuga nyuki wanawake wa Mayan akifungua mzinga, kutoka koloni la nyuki la Melipona huko Maní, Yucatán.

 

Bidhaa wanazozalisha zinakuja kwa ujazo tofauti, kuna zenye ujazo mdogo ambazo ni rahisi mtu kutembea nazo kwenye pochi au wakati akisafiri lakini pia zipo za ujazo mkubwa.

Kundi la wanawake wa Mayan wakiwa wamevalia nguo za kitamaduni zilizopambwa wakiwa wamesimama mbele ya kibanda chenye paa la nyasi.
© UNDP Mexico, SGP Mexico, Claudia Novelo Alpuche Mtandao wa wanawake wa Mayan wanaotengeneza asali ya melipona na kuhifadhi bionuai huko Mexico.