Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ladha tamu ya ufugaji nyuki wa kisasa Haiti :FAO 

Ilarion Celestin akikagua mizinga yake Bonbon, Haiti.
UN Haiti/Daniel Dickinson
Ilarion Celestin akikagua mizinga yake Bonbon, Haiti.

Ladha tamu ya ufugaji nyuki wa kisasa Haiti :FAO 

Ukuaji wa Kiuchumi

Wafugaji wa nyuki katika wilaya ya kusini mwa Haiti ya Bonbon wanazua gumzo kuhusu asali katika eneo ambalo linajikwamua baada ya tetemeko la ardhi la mwaka 2021. 

Ilarion Celestin, alipigwa jeki na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO na wizara ya mazingira ya Haiti kama sehemu ya mradi wa kupambana na kuenea kwa jangwa ili kufanya uzalishaji wake wa asali kuwa wa kisasa zaidi. 

Amezungumza na UN News kabla ya siku ya nyuki duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 20 Mei. 

Wafuga nyuki kutoka kusini mwa Haiti Bonbon wanazua gumzo kuhusu asali katika sehemu inayoibuka kutokana na tetemeko la ardhi.
UN Haiti/Daniel Dickinson
Wafuga nyuki kutoka kusini mwa Haiti Bonbon wanazua gumzo kuhusu asali katika sehemu inayoibuka kutokana na tetemeko la ardhi.

“Nilikuwa mfugaji nyuki wa kitamaduni. Nyuki wangu walitengeneza asali kwenye shina la mti lenye shimo, lakini Shirika la chakula na kilimo liliniunga mkono kubadili mfumo wa  zamani na kuingia wa kisasa wa ufugaji nyuki kwenye mafunzo ya kiufundi na vifaa vyote, ikiwa ni pamoja na mizinga 18, niliyohitaji kuwa mfugaji nyuki mwenye taaluma.” 

Ameendelea kusema kuwa tulijifunza jinsi ya kutunza nyuki vizuri na sasa wana afya bora na wanazalisha asali nyingi na uzalishaji ni wa usafi zaidi. 

Ninapenda asali ni nzuri kuonja na ina protini nyingi na pia ni dawa. Nyuki wangu hutengeneza aina nne tofauti za asali, ninachopenda zaidi ni kutoka kwa maua ya mti wa Moringa, ambayo yanatoa asali nyeupe. 

Kwa kutumia vifaa vya kisasa vya kufuga nyuki kiasi cha asali anachopata Ilarion Celestin.
UN Haiti/Daniel Dickinson
Kwa kutumia vifaa vya kisasa vya kufuga nyuki kiasi cha asali anachopata Ilarion Celestin.

Nyuki hufanya kazi ngumu 

Kwangu mimi sio kazi ngumu, anasema Ilarion , mimi huangalia kila mzinga mara mbili kwa mwezi na kuvuna asali mara tatu kwa mwaka. Ni nyuki wanaofanya kazi ngumu. 

Mavuno yangu ya asali yameongezeka kutoka karibu galoni mbili kwa mwaka nilipochunga nyuki kwa njia ya kitamaduni, hadi karibu galoni 270 na bila shaka, maisha yangu yamebadilika kabisa kama matokeo ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa. 

Ninaweza kupata pesa nzuri sana. Galoni moja inauzwa karibu  dola $50, kwa hivyo ni biashara nzuri.  

FAO inatuambia kuna uhitaji mkubwa wa asali na pengine katika siku zijazo, mazao yangu yatauzwa nje ya nchi. Hivi sasa, ninaiuza ndani ya nchi na katika mji mkuu wa Port-au-Prince. 

Sasa ninaweza kumudu kuwapeleka watoto shule, kujenga nyumba yangu na kununua ng'ombe. 

Watu wengi zaidi wameanza kuwa na nia ya kuwa wafugaji nyuki, hasa tangu tetemeko la ardhi lilipotokea Agosti 2021.  

Nilifunzwa na FAO kufundisha watu wa eneo hilo na wanakuja shambani kwangu kuona jinsi ninavyoendesha biashara yangu, kwa hiyo ninaongoza vipindi vingi vya mafunzo na ninahisi vizuri kushiriki ujuzi na uzoefu wangu na wengine.  

Sasa kuna wafugaji nyuki wapatao 60 wanaozalisha asali katika eneo hili. 

Wafugaji hawa wapya wanatambua kuwa hata tetemeko la ardhi haliwezi kuwavuruga nyuki wanaotengeneza asali, ingawa baadhi ya wakulima katika ushirika wangu walipoteza baadhi ya nyuki wakati mizinga yao ilipoanguka kutokana na tetemeko la ardhi la Agosti mwaka jana na bila shaka pia kuna hatari ya maporomoko ya ardhi,  lakini, kwa ujumla, hii ni kazi nzuri kwa siku zijazo. 

Wakulima wanachangia katika kupanda miti nchini Haiti.
WFP Haiti/Theresa Piorr
Wakulima wanachangia katika kupanda miti nchini Haiti.

 

Changamoto ya mabadiliko ya tabianchi 

Changamoto kuu inayotukabili ni mabadiliko ya tabianchi. Tunapokuwa na ukame maua kwenye miti hayakui vizuri na kuna maji kidogo, hivyo nyuki wanapaswa kusafiri mbali zaidi kukusanya nekta na kunywa maji, hali ambayo inamaanisha kwamba hutoa asali kidogo. 

Kwa hivyo, naanza kupanda miti na kuhakikisha kuwa wana maji ya kutosha. Kwa njia hii, ninaunga mkono pia urejeshaji wa ndani wa misitu ambayo ni mizuri kwa jamii yangu kwani inapunguza mmomonyoko wa udongo hali ambao wakulima wanaitumia kulima mazao na kuna ongezeko la bioanuwai.