Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchunguzi kuhusu COVID-19 wahimiza ujasiri wa hatua za kuzuia janga hilo:WHO 

Wahudumu wa afya na wafanyakazi wengine wa mstari wa mbele katika Wilaya ya Gorkha kaskazini kati mwa Nepal wakipokea dozi ya pili ya COVID-19.
© UNICEF/Preena Shrestha
Wahudumu wa afya na wafanyakazi wengine wa mstari wa mbele katika Wilaya ya Gorkha kaskazini kati mwa Nepal wakipokea dozi ya pili ya COVID-19.

Uchunguzi kuhusu COVID-19 wahimiza ujasiri wa hatua za kuzuia janga hilo:WHO 

Afya

Jopo la ngazi ya juu lililoteuliwa na Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, leo limehimiza kuchukuliwa hatua za kijasiri ili kumaliza janga la corona au COVID-19, huku pia likitaka shirika hilo la Umoja wa Mataifa lipewe mamlaka zaidi ya kuchukua hatua za haraka zaidi kwa vitisho vya siku zijazo vya milipuko ya majanga kama hili.

"Ujumbe wetu ni rahisi na wa wazi, mfumo wa sasa umeshindwa kutukinga na janga la COVID-19. Ikiwa hatutachukua hatua za kuibadilisha mfumo huo sasa, hautoweza kutulinda na tishio la janga litakalokuja, ambalo linaweza kutokea wakati wowote."  Amesema Rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, a,mbaye ni mwenyekiti mwenza wa Jopo hilo huru la kujiandaa na kupambana na majanga. 

Jopo hilo lililozinduliwa na mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, ni jopo huru lilitoa matokeo na mapendekezo yake baada ya mapitio ya miezi minane ya mambo tuliyojifunza kutoka na janga hilo kwa mwaka uliopita. 

Ulinzi usiotosheleza 

"Zana hizo zinapatikana ili kumaliza magonjwa hatari, vifo, na athari za kijamii na kiuchumi zilizosababishwa na COVID-19. Hakuna chaguobali kuchukua hatua  kuzuia janga kama hilo kutokea tena.”amesema mwenyekiti mwenza wa jopo hilo Helen Clark, Waziri mkuu wa zamani wa New Zealand, akisisitiza  kwa viongozi kwamba "Mfumo wa sasa  katika viwango vya kitaifa na kimataifa haukutosha kulinda watu kutokana na janga la COVID-19. Muda uliochukua hadi kutoa ripoti za homa ya mapafu ya asili isiyojulikana katikati ya mwishoni mwa Desemba 2019 hadi  kutangazwa kuwa dharura ya afya ya Umma ya wasiwasi wa Kimataifa ilikuwa muda mrefu sana, "jopo lilisema katika taarifa yaowaliyoiita “COVID -19: ifanye kuwa janga la mwisho.” 

Vijana wanaojitolea nchini Jordan katika jamii zao wakati huu wa janga la COVID-19
© UNICEF/Naua
Vijana wanaojitolea nchini Jordan katika jamii zao wakati huu wa janga la COVID-19

Mwezi mzima ulipotea 

Jopo hilo ambalo ripoti yake ina "mpangilio wa maalum wa kile kilichotokea" pia ilisisitiza kuwa Februari 2020 ilikuwa ni "mwezi uliopotea". 

Hii ni kwa sababu nchi nyingi zaidi zingeweza kuchukua hatyua zaidi kuzuia kuenea kwavirusi vipya vya corona baada ya WHO kutangaza dharura ya afya ya umma ya wasiwasi wa kimataifa hapo 30 Januari, baada ya mlipuko wa kwanza kuzuka huko Wuhan, Uchina. 

Rafu za vyumba vya kuhifadhia nyaraka kwenye umoja wa Mataifa na miji mikuu ya kitaifa zimejaa ripoti na hakiki za majanga ya kiafya yaliyopita.  

“Endapo maonyo yao yangezingatiwa, tungeepuka maafa tuliyo nayo leo. Wakati huu lazima uwe tofauti, ”amesema Bi. Johnson Sirleaf. 

Ulinzi usiofaa

Hatua ya haraka "zingesaidia kuzuia janga la kiafya, kijamii, na kiuchumi ambalo linaendelea kushika kasi", jopo limebaini, na kuongeza kuwa ni dhahiri "mfumo uliopo sasa haufai kuzuia janga lingine na virusi vinavyoambukiza na kusambaa sana, ambavyo vinaweza kuibuka wakati wowote, na kuwa janga ”.
Miongoni mwa mapendekezo ya jopo hilo na baada ya kuonyesha jinsi shida ya virusi vya corona inavyoendelea kuangamiza jamii, jopo hilo liliwataka wakuu wa nchi kuongoza katika kuunga mkono hatua zilizothibitishwa za afya ya umma kukabiliana na janga hilo na kutekeleza mageuzi "ili kuzuia kuzuka kwa janga kama hilo kwa siku zijazo na kuenea ulimwenguni kote.”

Muhudumu wa afya akimchanja mtu wa pili kupata chanjo ya COVID-19 nchini Angola kwa mfumo wa COVAX.
© UNICEF/COVAX/Carlos César
Muhudumu wa afya akimchanja mtu wa pili kupata chanjo ya COVID-19 nchini Angola kwa mfumo wa COVAX.


Wito wa dozi bilioni moja

Jopo pia limezishauri nchi zenye kipato cha juu na ugavi wa chanjo ya kutosha kujitolea kutoa "angalau dozi bilioni moja" kwa nchi 92 za kipato cha chini na cha kati katika mpango wa chanjo unayoongozwa na Umoja wa Mataifa, COVAX, ifikapo Septemba 2021.
Nchi kubwa zinazozalisha chanjo na makampuni ya uzalishaji wanapaswa kukubali kushirikiana haki miliki kwenye chanjo zao, lilisema jopo likiongozwa na shirika la afya laUmoja wa Mataifa na shirika la biashara duniani (WTO).
Endapo hatua juu ya suala hili hazitatokea ndani ya miezi mitatu, kuondolewa kwa haki miliki chini ya mkataba wa vipengele vinavyohusiana na biashara ya haki miliki zinapaswa kuanza kutumika mara moja", limesisitiza jopo hilo.
Likizigeukia nchi tajiri zaidi ulimwenguni, zinayojulikana kama G7, jopo hilo la wataalam wanaoongoza limependekeza kwamba "mara moja waongeze asilimia 60 ya dola bilioni 19 zinazohitajika kwa Upataji wa nyenzo za kusongesha zana za kupambana na COVID-19 kwa chanjo, uchunguzi, matibabu, na uimarishaji wa mifumo ya afya.”

Chanjo dhidi ya COVID-19 ni msingi wa kukabili janga la corona
Unsplash/Ivan Diaz
Chanjo dhidi ya COVID-19 ni msingi wa kukabili janga la corona


Wito wa mkutano

Wakuu wa Serikali wanapaswa kujitolea kwa mageuzi haya katika mkutano wa kimataifa, jopo liliendelea kusena kwa kupitisha azimio la kisiasa chini ya usimamizi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Kuelezea mapendekezo yake kama "mabadiliko", jopo limeonyesha kwamba wale wasio na uwezo wa kuhimili majanga , wengi ndio wameathirika zaidi.
"Hadi watu milioni 125 wanakadiriwa kusukumwa katika umaskini uliokithiri, wakati watoto milioni 72 zaidi wa umri wa kwenda shule za msingi sasa wako katika hatari ya kushindwa kusoma au kuelewa maandishi rahisi kwa sababu ya kufungwa kwa shule," wataalam walibaini.
Wanawake pia wamebeba mzigo mkubwa, wakiendelea kukabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia katika viwango vilivyovunja rekodi ya juu na ndoa za utotoni zinaongezeka.

Wafanyabiashara katika solo la Luanda angola, wamechukua hatua za kujilinda wakati wa janga la COVID-19
© FAO/ C. Marinheiro
Wafanyabiashara katika solo la Luanda angola, wamechukua hatua za kujilinda wakati wa janga la COVID-19


Wakisisitiza mshtuko wa kiuchumi wa mwaka wa jana, wataalam pia wamegundua kuwa ulimwengu "ulipoteza dola trilioni 7" katika pato la uchumi zikiwa ni zaidi ya pato la taifa la mwaka 2019 la bara lote la Afrika ($ 6.7 trilioni) ".
Ongezeko la karibuni la wagonjwa
Kwa mujibu wa WHO kumekuwa na zaidi ya visa milioni 159 vilivyothibitishwa vya COVID-19 duniani, pamoja na vifo zaidi ya milioni 3.3 tangu janga hilo lianze. 
Katika toelep lake la kila wiki kuhusu janga hilo linavyoendelea, shirika la afya la Umoja wa Mataifa limebaini kuwa jumla ya chanjo bilioni 1.2 zimetolewa. 
Idadi ya wagonjwa wapya na vifo vya COVID-19 ulimwenguni imepungua kidogo katika wiki iliyopita, kukiripotowa zaidi ya wagonjwa milioni 5.5 na zaidi ya vifo 90,000. 
Hata hivyo WHO imeonya kuwa "idadi ya wagonjwa na vifo ipo katika viwango vya juu kabisa tangu mwanzo wa janga hilo". 
Kesi mpya za wagonjwa wa kila wiki zimepungua Ulaya na Mashariki mwa Mediterania, wakati ukanda ka Kusini-Mashariki mwa Asia wagonjwa wameendelea kuongezeka, ukiripoti ongezeko la zaidi ya asilimia sita kwa kipindi cha siku saba zilizopita.