Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miongo 3 ya vita dhidi ya amabadiliko ya tabianchi, COVID-19 imetuweka njiapanda:UN

Barafu katika bahari ya Bellingshausen Antarctica
WMO/Gonzalo Bertolotto
Barafu katika bahari ya Bellingshausen Antarctica

Miongo 3 ya vita dhidi ya amabadiliko ya tabianchi, COVID-19 imetuweka njiapanda:UN

Tabianchi na mazingira

Kwa miaka 28, na kwa wasiwasi unaoongezeka, wanasayansi wakitumia takwimu wamekuwa wakionya juu ya mabadiliko ya tabianchi na athari zake. 

Mwaka 2020, ongezeko la joto duniani liliendelea kupanda, pamoja na majanga ambayo yanajumuisha mvua kubwa na ukame, moto, kupanda kwa vina vya bahari, na kati ya mambo mengine, kukawa na msimu wa aina yake wa vimbunga katika ukanda wa Karibbea kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa. 
Ripoti hiyo ya shirika la hali ya hewa diuniani WMO inasema jnga la corona au COVID-19 limezidisha zaidi njaa, umaskini na na watu kutawanywa  kulikosababishwa na mabadiliko ya tabianchi katika mwaka ambao ulitikisa dunia.
Mabadiliko mabaya ya tabianchi pamoja na janga la COVID-19 vimekuwa msumari wa moto juu ya kidonda kwa mamilioni ya watu kwa mwaka 2020, lakini hata kudorora kwa uchumi kunakohusiana na janga hilo kulishindwa kuwazuia vichocheo vya ongezeko la joto duniani na athari zake za kuongeza kasi, imesema ripoti hiyo mpya ya WMO.
Ripoti hiyo ambayo ni ya kila mwaka ya “Hali ya mabadiliko ya tabianchi duniani” inathibitisha kuwa mwaka 2020 ulikuwa moja ya miaka mitatu yenye joto zaidi katika historia, licha ya hali ya kupoza kawaida iliyosababishwa na  La Niña ambayo lilikuwepo. 
Joto la wastani duniani mwaka huo lilikuwa karibu nyuzi joto 1.2 ° Celsius juu ya kiwango cha kabla ya mapinduzi ya viwanda (1850-1900).
Kwa kuongezea, ripoti inasema miaka sita tangu 2015 imekuwa ya joto zaidi kwenye rekodi, na 2011-2020 ulikuwa muongo wenye joto zaidi kkatika historia.

Barafu ikielea juu ya maji katika eneo la Prince Gustav Antarctica
WMO/Gonzalo Javier Bertolotto Quintana
Barafu ikielea juu ya maji katika eneo la Prince Gustav Antarctica


Mkuu wa WMO Talas

Akizungumzia hali hiyo katibu mkuu wa WMO Peterri Talas amesema “Imekuwa ni miaka 28 tangu shirika la hali ya hewa duniani lilipotoa ripoti yake ya kwanza kuhusu hali ya hewa duniani mnamo 1993, kwa sababu ya wasiwasi ulioibuliwa wakati huo kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Tuna miaka 28 ya takwimu zinazoonyesha ongezeko kubwa la joto duniani na baharini, pamoja na mabadiliko mengine kama vile kuongezeka kupanda kwa vina vya bahari, kuyeyuka kwa barafu ya bahari na theluji, na mabadiliko katika mifumo ya mvua. Hii inasisitiza uimara wa sayansi ya hali ya hewa kulingana na sheria za asili zinazosimamia tabia ya mfumo wa hali ya hewa.”

Ameongeza kuwa wataalam wamesisitiza kuwa viashiria vyote muhimu vya hali ya hewa na habari vinayotolewa na ripoti hiyo vinaonyesha mabadiliko ya tabianchi yasiyokoma na endelevu, tukio linaloongezeka kwa hafla na matukio mabaya ya hali ya hewa yanayoathiri watu wengi, jamii na uchumi.

"Mwelekeo mbaya wa hali ya hewa utaendelea kwa miongo ijayo bila kujali mafanikio yetu ya kupunguza. Kwa hivyo, ni muhimu kuwekeza katika hali ya kuukabili. Hivyo njia mojawapo ya yenye nguvu ya kujenga mnepo ni kuwekeza katika huduma za utoaji taarifa za taahadhari  mapema na mitandao ya uchunguzi wa hali ya hewa. Nchi kadhaa ambazo hazijaendelea sana zina mapungufu muhimu katika mifumo yao ya uchunguzi na zinakosa huduma za hali ya juu za hali ya hewa, hali ya hewa na huduma za maji. “ameonya mkuu wa shirika hilo la la Umoja wa Mataifa

Moto wa nyika ukiteketeza eneo huko California Marekani mwaka 2018
Peter Buschmann for Forest Service
USDA
Moto wa nyika ukiteketeza eneo huko California Marekani mwaka 2018


COVID-19 imeongeza adha ya mabadiliko ya tabianchi 2020

Mwaka 2020, COVID-19 iliongeza mwelekeo mpya na usiohitajika wa mabadiliko ya tabianchi, hali ya hewa na hatari za maji, na pia athari kubwa kwa afya ya binadamu na ustawi, imeeleza ripoti hiyo ambayo imeangazia mwaka 2020.
Vizuizi vya uhamaji, kuporomoka kwa uchumi, na usumbufu katika sekta ya kilimo uliongeza athari za matokeo ya mabadiliko ya tabianchi katika mfumo mzima wa usambazaji wa chakula, kuongeza viwango vya ukosefu wa chakula na kupunguza kasi ya utoaji wa misaada ya kibinadamu. 
Janga hilo pia lilivuruga uchunguzi wa hali ya hewa na juhudi ngumu za kupunguza hatari za majanga.
Ripoti hiyo, ambayo inakusanya pamoja tafiti kutoka kwa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa, inaonyesha jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyokuwa hatari katika kufanikiwa kwa malengo mengi ya maendeleo endelevu, SDGs kupitia mlolongo wa matukio yanayohusiana. Hizi zinaweza kuchangia kuimarisha au kuzidisha usawa uliopo. 
Kwa kuongezea, ripoti inasema kuna uwezekano wa vitanzi vya maoni ambavyo vinatishia kuendeleza mzunguko mbaya wa mabadiliko ya

tabianchi.

Maelfu ya watu nchini Somalia wanaedelea kukimbia kutokana na mafuriko na mizozo.
UN Photo/Tobin Jones)
Maelfu ya watu nchini Somalia wanaedelea kukimbia kutokana na mafuriko na mizozo.


Mwaka 2021 ni mwaka muhimu sana -Guterres

Talas amewasilisha ripoti hiyo kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Ripoti hiyo imetolewa kabla ya mkutano wa viongozi utakaofanyika kwa njia ya mtandao kuanzia Aprili 22-23, ulioitishwa na Marekani.
Rais Joe Biden anajaribu kuimarisha juhudi za taifa hilo la uchumi mkubwa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na kufikia malengo ya mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi ambayo yanataka kuhakikisha ongezeko la joto haliongezeki Zaidi ya  chini ya 2 ° C juu ya viwango vya kabla ya viwanda mwishoni mwa karne, na kwa 1.5 ° C ikiwezekana.
Mwisho wa mwaka, Mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, au COP26, utafanyika nchini Uingereza, mkutano wa kimataifa ambao Guterres ameielezea kama umuhimu wake ni "dhahiri."

 “Ripoti hii inaonyesha kuwa hatuna muda wa kupoteza. Hali ya hewa inabadilika na athari tayari ni za gharama kubwa kwa watu na sayari yetu. Huu ni mwaka wa utekelezaji. Nchi lazima zijitoe kimasomaso kuhakikisha hazizalishi kabisa hewa ukaa ifikapo mwaka 2050. Lazima ziwasilishe, kabla ya mkutano wa COP26 huko Glasgow, mipango kabambe ya kitaifa ya mabadiliko ya tabianchi ambayo kwa pamoja itapunguza uzalishaji wa hewa ukaa duniani kwa asilimia 45% ikilinganishwa na viwango vya mwaka 2010 ifikapo mwaka 2030. Na ni lazima wachukue hatua sasa kulinda watu dhidi ya maafa na athari za mabadiliko ya tabianchi”, ameonya Katibu Mkuu.

Mafuriko nchini Chad yanasababisha madhila kwa wakazi nchini Chad.
IOM/Adeline Tannone
Mafuriko nchini Chad yanasababisha madhila kwa wakazi nchini Chad.

Takwimu za ripoti

Ongezeko la gesi chafuzi za viwandani liliendelea kuongezeka mwaka 2019 na 2020. Wastani wa chembechembe za molekuli za hewa ukaa (CO2) ulimwenguni tayari vimevuka sehemu 410 kwa milioni moja (ppm), na ikiwa mkusanyiko wa hewa ukaa unafuata muundo ule ule kama katika miaka ya nyuma, inaweza kufikia au kuzidi sehemu 414 ppm mwaka huu wa 2021.
Kudorora kwa uchumi kwa muda kulisababisha uzalishaji mpya wa gesi chafuzi, kulingana na mpango wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa, lakini haukuwa na athari yoyote inayoonekana katika viwango vya anga.