Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yataka hatua Madhubuti kutatua changamoto ya madeni kwa nchi zinazoendelea 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia mkutano wa ngazi ya juu kuhusu madeniuliofanyika kwa njia ya mtandao
UN Photo/Eskinder Debebe)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia mkutano wa ngazi ya juu kuhusu madeniuliofanyika kwa njia ya mtandao

UN yataka hatua Madhubuti kutatua changamoto ya madeni kwa nchi zinazoendelea 

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Ingawa kuna hatua kubwa zimechukuliwa kuzuia mgogoro wa madeni ulimwenguni uliosababishwa na janga la corona au COVID-19, hatua hizo hazijatosha kurejesha utulivu wa kiuchumi katika nchi nyingi zinazoendelea, kulingana na tamko la kisera liliotolewa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. 

Antonio Guterres amesema zaidi ya mwaka mmoja tangu kuzuka kwa janga hilo, athari za kifedha za mgogoro huo zinasababisha shida ya madeni katika idadi kubwa ya nchi na zinazuia sana uwezo wa wengi, kuwekeza katika kujikwamua na janga hilo na kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), ikiwa ni pamoja na katika mabadiliko ya tabianchi yanayohitaji haraka hatua. 

Hali halisi ya madeni 

Kwa mujibu wa tamko hilo la kisera  uchumi  wan chi 42 unaokopa kutoka kwenye masoko ya mitaji zimeshuhudia kushuka kwa nguzu za uhuru wao tangu kuanza kwa janga la coronavirus">COVID-19 ikiwa ni pamoja na nchi 6 zilizoendelea, nchi 27 za uchumi unaoibuka, na nchi 9 zinazoendelea. 

Kuzorota kwa uwezo wa kujitawala husababisha gharama za kukopa kuongezeka, haswa kwa nchi zinazoendelea, ambazo zinaweza kuongeza hatari ya mataifa mengi kuchukua madeni wasiyoweza kudumu haswa ikiwa janga la COVID-19 litadumu kwa muda mrefu na kuleta athari za kina kuliko inavyotarajiwa. 

Mtu akiwa amebeba kiroba cha mzigo mgogoni katika mtaa kwenye pilika nyingi mjini Kathmandu Nepal. COVID-19 na amri zingine za kutotembea viewaathiri vibaya watu huku watu wengi wanaotegemea kibarua cha siku wakipoteza pato pekee wanalolitegemea
UN News/Vibhu Mishra

"Endapo hatutachukua hatua madhubuti juu ya changamoto za madeni na ukwasi, tunahatarisha kuwa na muongo mwingine uliopotea kwa nchi nyingi zinazoendelea, kuweka mafanikio ya utimizaji wa SDGs kwa tarehe ya mwisho ya 2030 njia panda ", amesisitiza Bwana Guterres. 

Tamko hilo la kisera, lililopewa jina la “Ufumbuzi wa kufilisika na  madeni Kuwekeza katika SDGs”, linaangalia hatua za kisera za ulimwengu tangu Aprili mwaka jana, kukagua mapungufu na changamoto zilizobaki za utekelezaji wao, na pia kupendekeza sasisho katika mapendekezo, yaliyowasilishwa mwaka jana, katika kufuatia mambo yaliyojitokeza katika miezi 12 iliyopita.