Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bahari na mustakbali wa dunia viko hatarini kutoka na mabadili ya tabianchi:WMO

Taa ikiangaza baharini pwani ya Florida nchini Marekani
Coral Reef Image Bank/David Gros
Taa ikiangaza baharini pwani ya Florida nchini Marekani

Bahari na mustakbali wa dunia viko hatarini kutoka na mabadili ya tabianchi:WMO

Tabianchi na mazingira

Katika kuelekea siku ya utabiri wa hali ya hewa duniani hapo kesho machi 23, shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO, limesema bahari huendesha hali ya hewa duniani na huimarisha uchumi na uhakika wa chakula. 

Lakini mabadiliko ya tabianchi yanaiathiri bahari na kuongeza hatari ya majanga kwa mamilioni ya watu duniani.

Kaulimbiu ya siku hiyo mwaka huu nia “Bahari, mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa”. Kwa mujibu wa WMO maudhui haya yanadhihirisha jinsi uchunguzi, utafiti na huduma vilivyo muhimu sasa kuliko kuliko hata awali ikizingatiwa kwamba zaidi ya asilimia 70 ya uso wa dunia unazidi kuwa hatarini kutokana na matukio yanayohusiana na hali ya hewa.

Hali ya Hewa na Mazingira

Mabadiliko ya hali ya hewa yamezathiri bahari za dunia kwa kiasi kikubwa, wataalam wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa wamesema leo  katika wito wa ufuatiliaji wa kuokoa maisha na huduma za utoaji tahadhari za mapema ambazo zilikatizwa na janga la corona au COVID-19 hivyo zinapaswa kuongezewa tena, kulinda usafirishaji kwa njia ya meli na jamii za pwani zilizo katika hatari zaidi.

Viwango vya hewa ukaa vinaendelea katika kiwango cha rekodi ya juu, licha ya kushuka kwa uchumi kusababishwa na janga la COVID-19.
Unsplash/Johannes Plenio
Viwango vya hewa ukaa vinaendelea katika kiwango cha rekodi ya juu, licha ya kushuka kwa uchumi kusababishwa na janga la COVID-19.

Katika tahadhari kwamba ongezeko la baharini  lilichangia kuongeza  kwa rekodi ya vimbunga  katika bahari ya Atlantiki mwaka jana, pamoja na vimbunga vikali vya kitropiki katika Bahari ya Hindi na Kusini mwa Pacific, limesema shirika la WMO pia lilisisitiza tishio la muda mrefu kutokana na  kupanda kwa kina cha bahari.

"Karibu asilimia 40 ya idadi ya watu ulimwenguni wanaishi ndani ya kilomita 100 kutoka pwani, kuna haja ya dharura ya kuzilinda jamii hizi kutokana na  hatari zinazokumba maeneo ya pwani, kama vile mawimbi, kuongezeka kwa dhoruba na kuongezeka kujaa kwa kina cha bahari kupitia mifumo ya utoaji wa tahadhari za mapema na utabiri “, amesema Profesa Petteri Taalas, Katibu Mkuu wa WMO.

Uchumi unaotegemea bahari

Kulingana na shirika la WMO "uchumi wa wa bahari” unakadiriwa kuwa dola trilioni 3-6  kwa mwaka, ukiwa ni zaidi ya robo tatu ya biashara yote ulimwengu na kutoa riziki kwa zaidi ya watu bilioni sita.

Mamilioni ya dola katika bidhaa na mamia ya maisha bado wanapotea baharini kila mwaka, kwa sababu ya hali mbaya ya hewa kama vile upepo mkali, mawimbi makubwa, ukungu, ngurumo, barafu baharini na kuganda kwa maji kutokana na baridi kali  limeongeza shirika hilo la WMO.

Pia limeilezea bahari bahari kama "mita ya dunia", inachukua na kubadilisha sehemu muhimu ya mionzi ya jua na kutoa joto na mvuke wa maji angani.

Ingawa mikondo mikubwa ya bahari huzungusha joto hili duniani, mara nyingi kwa maelfu ya kilomita, shughuli za kibinadamu zimezidi kuathiri usawa wa bahari na anga ya asili.

Shirika la WMO limedokeza ukweli kwamba bahari hunyonya zaidi ya asilimia 90 ya joto la angani  lililonaswa na gesi chafuzi ya viwandani, ambayo imekuja "kwa gharama kuwa wakati joto la bahari na mabadiliko katika mfumo wa bahari tayari yanavuruga mazingira ya baharini na watu wanaowaitegemea ”.

Athari hii "itaonekana kwa mamia ya miaka", mkuu wa WMO Taalas amerendelea kusema, kabla ya kuonyesha athari kubwa ya kuyeyuka kwa barafu ulimwengu kote, kupitia mabadiliko ya tabianchi na kuongeza kasi kupanda kwa kicha cha bahari.

Mkurugenzi wa Kanda ya Amerika ya Kaskazini, Kati na Caribbea
UN/Costa Rica/Danilol Mora
Mkurugenzi wa Kanda ya Amerika ya Kaskazini, Kati na Caribbea

"Mwaka wa 2020, shirikia hilo limesema kiwango cha barafu katika bahari ya Aktiki kilikuwa kati ya kiwango vya chini kabisa katika historia, kikiziweka jamii za Polar katika hatari ya mmafuriko yasiyo ya kawaida ya pwani, na wadau kama wasafirishaji na uvuvi, hadi kwa hatari zitokanazo na barafu za baharini,".

Uchunguzi wa vitisho

Kabla ya Siku ya utabiri wa hali ya hewa duniani hapo kesho Jumanne Machi 23, WMO imeonyesha thamani ya saa 24 za kazi kwa siku 7 kwa wiki  ya vituo vya kitaifa vya hali ya hewa katika kulinda maisha na mali sio tu ardhini bali pia baharini.

Ingawa usahihi na wakati wa utabiri wa hali ya hewa umeboreshwa, WMO imeelezea kuwa meli zilizokosa teknolojia ya kisasa mara nyingi zinasafiri bila habari hii muhimu ya usafirishaji.

"Ni muhimu kuboresha huduma za msaada wa maamuzi kusaidia mabaharia kufikia usawa kati ya kupunguza gharama na njia, lakini vilevile kuongeza usalama na kuepuka hali ya hewa ya baharini yenye hatari.”

Limeongeza kuwa kikubwa kinachotia hofu ni ongezeko la upotevu wa barafu baharini kutokana na ongezeko la joto duniani.

“Kuwa na barabu kidogo hakumaanishi hatari ni ndogo na athari ya ajali kwenye eneo la maji ya Arktiki itakuwa na madhara makubwa kwa mazingira .”

Hivyo WMO inajaribu kuboresha utabiri wa hali ya hew ana kutoa tahadhari ya mapema kwa hali ya hew ana hali ya barafu katika ukanda wa Aktiki.