Pole sana Watanzania kwa msiba, tuko pamoja:RC Zlatan

18 Machi 2021

Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Zlatan Milisic, amesema amestushwa sana na kifo cha Rais John Joseph Pombe Magufuli, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichotokea jana Jumatano Machi 17.

Kupitia taarifa yake iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es salaam leo Bwana. Milisic amesema “Kwa niaba ya familia ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania natoa salamu zangu za rambirambi za dhati kwa mjane wa Rais wa Tanzania Bi. Janet Magufuli, makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, wawakilishi wa serikali na wananchi wote wa Tanzania. Natoa pole zangu na kuwajulisha kwamba fikra zangu ziko pamoja nanyi.”

Mratibu huyo ameongeza kwamba familia ya Umoja wa Mataifa inaomboleza pamoja na Watanzania na kuwa itaendelea kufanyakazi kwa karibu na serikali kwa faida ya watu wa Jasmhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amehitimisha ujumbe wake kwa kumuomba mola aipumzishe kwa amani roho ya marehemu.

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter