Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bendera ya UN yapepea nusu mlingoti kumuenzi hayati Rais John Magufuli wa Tanzania

Bendera ya Umoja wa Mataifa ikipepea nusu mlingoti (Kutoka Maktaba)
UN Photo/Eskinder Debebe)
Bendera ya Umoja wa Mataifa ikipepea nusu mlingoti (Kutoka Maktaba)

Bendera ya UN yapepea nusu mlingoti kumuenzi hayati Rais John Magufuli wa Tanzania

Masuala ya UM

Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, bendera ya Umoja wa Mataifa inapepea kwa nusu mlingoti kuashiria maombolezo ya kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyefariki dunia tarehe 17 mwezi huu wa Machi.

Rais Magufuli aliaga dunia jijini Dar es salaam naamezikwa leo nyumbani kwake huko Chato mkoani Geita nchini Tanzania.

Hafla ya kushusha bendera hiyo nusu mlingoti kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani imeshuhudiwa na  Afisa kutoka ujumbe wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Songelael Shilla ambaye amesema ni utaratibu wa Umoja wa Mataifa kufanya hivyo anapofariki dunia mkuu wa nchi au serikali ambaye yuko madarakani