Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado nina wasiwasi na hali ya inayoendelea Sahel:Guterres 

Mnamo Februari 2020, mji wa Dori ukanda wa Sahel nchini Burkina Faso lilikuwa linahifadhi takriban wakimbizi wa ndani 15,000.
© UNHCR/Sylvain Cherkaoui
Mnamo Februari 2020, mji wa Dori ukanda wa Sahel nchini Burkina Faso lilikuwa linahifadhi takriban wakimbizi wa ndani 15,000.

Bado nina wasiwasi na hali ya inayoendelea Sahel:Guterres 

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema licha ya maendeleo yaliyopatikana hivi karibuni katika mchakato wa amani na pia kufanyika kwa chaguzi kwa njia ya amani bado ana wasiwasi kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama Sahel hasa katika katika maeneo ya Liptako-Gourma ambako kuongezeka kwa machafuko kumefanya hali ya kibinadamu kuwa mbaya zaidi. 

Antonio Guterres amesema hayo kupitia ujumbe wake wa video kwenye mkutano wa wakuu wan chi za ukanga wa Sahel au G5 zinazojumuisha Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania na Niger, unaofanyika leo kwenye mji mkuu wa Chad, N’Djamena. 

Katika mkutano huo ambao Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anahudhuria pia kwa njia ya mtandao, Katibu Mkuu amesema “Mara nyingi kunapozuka machafuko raia ndio wanaolipa gharanma kubwa,  zaidi ya watu milioni 2 wamelazimika kukimbia makwao, mamilioni wengine hawakabiliwa na uhaba wa chakula na ukichanganya na mabadiliko ya tabianchi hali inazidi kubwa tete kwao.” 

Pia amesema janga la corona u COVID-19 limeongeza adha kwa watu wa ukanda wa sahel , ukiongeza na changamoto za kiuchumi na kiafya za janga hilo zimefanya watu wengine milioni 6 kusukumwa kwenye umasikini. 

G5 ina wajibu wa kutatua shida hii 

Bwana. Guterres amesisitiza kwamba nchi za G5 zina wajibu mkubwa wa kughulikia changamoto hizi. 

Mwaka mmoja baada ya mkutano Pau kikosi cha pamoja cha nchi hizo kinaendelea kukua kutokana na uhamasishaji wan chi hizo , msaada kutoka kwa washirika wa kimataifa na msaada wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali , MINUSMA ameongeza Katibu Mkuu. 

“Ninashukuru nchi zilizohusika na upelekeji wa kikosi kazi cha Takuba kilichoundwa na vikosi maalum vya Ulaya kwa kufuata utaratibu wa Sahel G5 kwani hii inaonyesha uhamasishaji na mshikamano.” 

Ameongeza kuwa hali hiyo inapaswa kudumishwa hasa wakati huu ili kudhihirisha uheshimuji wa haki za binadamu na hilo amehimiza kuwa kikosi hicho cha pamoja kinahitaji kuwa fedha endelevu ili kutimiza wajibu wake ipasavyo. 

Kuhusu suala la ugaidi katika ukanda huo Guterres amesema “Operesheni za amani na vita dhidi ya ugaidi Afrika lazima ziidhinishwe na Baraza la Usalama la Umoja kwa kuzingatia kufungu namba VII, ufadhili wa operesheni hizo na michango ya lazima kutoka kwa nchi wanachama..” 

Pia amesisitiza kwamba msaada wa MINUSMA kwa mchakato wa amani na utulivu Mali ni lazima uwe kipaumbele kwa nchi wanachama wa Sahel G5. 

Ukosefu wa usalama na ukame vimesababisha njaa ukanda wa Sahel na kulazima mashirika ya Umoja wa Mataifa kama WFP kulazimika kugawa mlo kwa wakazi wa eneo hilo.
WFP/Sébastien Rieussec
Ukosefu wa usalama na ukame vimesababisha njaa ukanda wa Sahel na kulazima mashirika ya Umoja wa Mataifa kama WFP kulazimika kugawa mlo kwa wakazi wa eneo hilo.

Mashambulizi dhidi ya walinda amani 

Bwana. Guterres amelaani vikali mashambulizi ya uwoga yanayofanywa dhidi ya walindamani wa Umoja wa Mataifa akikumbusha shambulio la hivi karibuni lililofanyika wiki iliyopita na kutoa wito kwa mamlaka ya nchi hiyo kujitahidi kadri ya uwezo wake kuwabaini wahalifu hao na kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria. 

Pia amesisitiza kwamba “Mbali ya suala la usalama, maendeleo, utawala wa sheria na utawala bora ndio msingi wa utulivu katika ukanda wa Sahel. Serikali lazima zirejeshe imani kwa raia wake na tumeazimia kuunga mkono juhudo zote katika mwelekeo hu una pia vyanzo vya migogoro na changamoto ingine lazima vishughulikiwe.” 

Ameongeza kuwa mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo Sahel Mar Dieye atahakikisha kwamba uhusiano kati ya binadamu, mabadiliko ya tabianchi, usalama, siasa na changamoto za maendeleo vinazingatiwa kwa njia iliyo jumuishi na yenye ufanisi zaidi akijumuisha wadau wote husika akiwemo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu Afrika Magharibi na sahel Mohammed Chambas ili kutekeleza mkakati jumuishi wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Sahel  na kuunga mkono juhudi za G5.