Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa pendekezo ya kufuatilia wagonjwa wanaosalia na dalili baada ya kuugua COVID-19

Daktari akifuatilia mgonjwa waliye na COVID-19 Chernivtsi, Ukraine.
© UNICEF/Evgeniy Maloletka
Daktari akifuatilia mgonjwa waliye na COVID-19 Chernivtsi, Ukraine.

WHO yatoa pendekezo ya kufuatilia wagonjwa wanaosalia na dalili baada ya kuugua COVID-19

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya Ulimwenguni, WHO limetoa pendekezo kwamba wagonjwa waliougua ugonjwa wa virusi vya corona au COVID-19 wanaoshukiwa au waliothibitishwa wanahitaji kuwa na huduma ya baada ya matibabu iwapo wanadalili zisizoisha, mpya au zinazobadilika.

Hii ni moja ya mapendekezo ya WHO katika muongozo mpya wa matibabu.

Utafiti umethibitisha kwamba ugonjwa baada ya COVID-19 au COVID-19 ya muda mrefu ambako watu ambao wamepona kutoka kwa COVID-19 wanaendelea kuwa na changamoto za muda mrefu kama vile uchovu kupindukia, kikohozi cha muda mrefu na kushindwa kufanya mazoezi.

Kuelewa ugonjwa huu ni moja ya vipaumbele vya WHO ambapo kufikia Februari 2021, WHO itaratibu majadiliano kwa ajili ya kuafikiana kuhusu maelezo ya hali hiyo na aina zake. Uelewa wa kisiasa utaonogza jina la hali hiyo ambako majadiliano yanajumuisha washikadau mabli mbali ikiwemo makundi ya wagonjwa.

WHO inapendekeza matumizi ya vipimo vya viwango vya oxijeni kwenye damu kwa wagonjwa walio nyumbani na pia elimu kwa mgonjwa na mtoa huduma na kufuatiliwa kwa mgonjwa.

Kwa wagonjwa walio hospitalini, WHO inapendekeza matitbabu kuzuia kuganda kwa damu. Aidha kwa wagonjwa wanaopokea oxijeni, WHO inapendekeza kulaza wagonway kifudifudi ili kuhakikisha kutembea kwa oxijeni.