COVID-19 imedunisha zaidi maisha ya wanaofanyia kazi nyumbani:ILO

13 Januari 2021

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO, imesema ongezeko la watu kufanyia kazi majumbani kutokana na janga la corona au COVID-19 limedhihirisha mazingira duni ya kazi ambayo wafanyakazi wengi ambao wamekuwa wakifanyiakazi nyumbani hata kabla ya janga hilo wanayapitia na sasa inataka walindwe.

Kwa mujibu wa makadirio ya ripoti hiyo ya ILO“kufanyia kazi nyumbani, kutojulikana hadi ajira zenye hadhi”  takriban watu milioni 260 walikuwa wanafanyia kazi nyumbani duniani kote wakiwakilisha asilimia 7.9 ya ajira zote duniani, na asilimia 56 kati yao au sawa na watumilioni 147 walikuwa wanawake.  

Wafanyakazi hao walijumuisha wale ambao wanafanyia kazi nyumbani kila wakati na idadi kubwa ya wafanyakazi ambao wanahusika katika kazi za uzalishaji bidhaa ambazo haiwezi kufanyika kwa mtandao kama vile ushonaji, kazi za Sanaa , na kuunda vifaa vya kielektroniki. 

Na kundi la tatu ni wafanyakazi wa jukwaa la kidijitali ambao hutoa huduma kama vile kushughulikia madai ya bima, kuhariri nakala au kunyanyambua data kwa ajili ya mafunzo ya mifumo ya akili bandia. 

Kufuatia COVID-19 ripoti inasema sasa idadi ya wanaofanyia kazi nyumbani imeongezeka mara dufu na wafanyakazi hao wanahitaji ulinzi bora kwani kufanyiakazi nyumbani huwa ni kwa faragha na mara nyingi wafanyakazi hawaonekani. 

Ripoti imeongeza kuwa katika nchi za kipato cha chini na cha wastani kwa mfano karibu wafanyakazo wote wanaofanyiakazi nyumbani (asilimia 90) wanafanyakazi katika sekta isiyo rasmi nakwamba,  Kwa kawaida hali zao ni mbaya kuliko wanaofanyiakazi nje ya majumbani kwao. Hata katika nchi zenye watu wenye ujuzi wa hali ya juu wanalipwa kwa wasstani asilimia 13 chini yaw engine nchini Uingereza , Marekani asilimia 22 chini, Afrika Kusini asilimia 25 na karibu asilimia 50 chini nchini Argentina, India na Mexico.” 

Pia watu hao wanaofanyiakazi nyumbani hukabiliwa na hatari kubwa ya usalama na kiafya na wana fursa ndogo ya kupata mafunzo ikilinganishwa na wanaoenda maofisni hali ambayo inaweza kuathiri matarajio na mafanikio ya ajira zao. 

Katika miaezi ya kwanza ya janga la COVID-19 mwaka 2020 ripoti inakadiria kwamba mtu 1 kati ya 5 alijikuta analazimika kufanyiakazi nyumbani. 

Mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo na afisa wa masuala ya uchumi wa ILO Janine Berg amesema changamoto kubwa katika nchi nyingi ni kwamba kazi za kufanyia nyumbani hazina utaratibu maalum na sheria zilizopo haziwalindi kwani wengi huchukuliwa kama wafanyakazi binafsi na hivyo kutolewa kwenye kundi la sheria za ajira. 

Ma mantiki hiyo amependekeza kwamba “Serikali, wafanyakazi na mashirika ya waajiri wanapaswa kushirikiana pamoja kuhakikisha kwamba watu wote wanaofanyiakazi nyumbani iwe wanashona vikapu Indonesia, wanatengeneza mafuta Ghana, wanasafisha picha Misri, wanashona barakoa Uruguay au wanafanyiakazi mtandaoni Ufaransa, wanapaswa kutoka na kuzigeuza kazi hizo zisizoonekana na kuwa ajira zenye hadhi.” 

 

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud